Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Kwa kweli picha iliyoonyeshwa na TFF na Serikali katika kuthamini mchango wa wachezaji wa Stars katika kutuletea furaha Watanzania ni kuwa hata yaliyofanywa na Kamati eti ya hamasa ni kutafuta sifa binafsi na kutumia nguvu na uvumilivu wa vijana hawa kujijenga kisiasa tuu lakini sio kwa nia njema.
Iweje wamsahau kijana Shomari Kapombe? Kijana kapigana michezo yote ya awali hadi kuumia mazoezini Afrika Kusini na bado katika orodha ya zawadi anasahaulika?
Yaani kweli mpaka Kapteni wa Taifa Stars Mbwana Samatta anaamua kugawana zawadi zake na mchezaji wake ni AIBU ILIOJE? Ina maana hata TFF haijui Kapombe kafanya nini? mbona kuna wachezaji wengine wameongezwa mechi ya mwisho na pengine hawakucheza kabisa lakini wamelamba zawadi na kuachwa mpiganaji aliyeumia akiwa vitani?
Haya yote yametokana na kuingiza kamati za kisiasa na upigaji hela tuu, huwezi kusema Jina la Kapombe wamesahau kwa bahati mbaya bali nikuwa walikuwa hawajui kabisa yuko wapi na pengine hata matibabu yana hudumiwa na Club yake pekee.
Hongera Samatta kwa kuwaumbua hawa wababaishaji wanaongojea wengine wamenyeke wao waje kujibebea sifa za bure.