Hii ni biashara ya ukweli au?

Upanga

Senior Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
145
Reaction score
50
Ndugu zangu habari za Leo!Ningependa kuwaauliza kuhusu biashara ta RED MERCURY(ZEBAKI NYEKUNDU).
Nimepata taarifa kuwa hii kitu inatafutwa miaka nenda miaka rudi je ni kweli kitu kama hiii ipooooo?
Na nimeambiwa kuwa ukifanikiwa kuipata bei yake huwa ni kubwa je kuna ukweli?Naomba kuwasilisha
 
upanga
Member
Join Date: Mon Jun 2007
Posts: 15
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 3 Posts
Kwanza karibu sana jamvini baada ya kupotelea huko porini kusaka madini ya RED MERCURY!

Langu ni angalizo tu:
Angalia, usije ukatapeliwa, maana tangu ulipoondoka mjini ni siku nyingi..huh!
 
Yaani mimi binafsi sijaona mtu akawa tajiri kwa kuuza hiyo kitu ingawa nafahamu wengi wanaopata utajiri kwenye madini mengine!!!!
Nina brother wangu yaaaaani anaamini kupita kiasi kuwa hiyo biashara ipo na anajitahidi sana kupata angalau 10grms ili apate kutoka.
Nimemshauri nakumuuliza sana kama kuna mtu yeyote anayemfahamu kafanikiwa hana jibu lakini IMANI anayo kupita kiasi kama kuna mtu anafahamu biashara hiii ipo naomba anipe fununu tuuuuu!
 
hiyo kitu ipo sana ila inamatapeli wa kufa mtu watakwambia kuna sehemu inatoka matone matone kuna ya kutengeneza sajawahi kuona aliyefanikiwa kwenye hilo ilanilishawai kuingizwa town nikastuka
 
Wengine utawasikia sijui KARABAI ya mkoloni,,mara sijui Gwara lenye picha ya Trekta..
Watu tu wanahangaika,,ila ukimuuliza nani katoka kwa hiyo deal,,,hakuna jawabu..
Upanga kuwa muangalifu...
 
Nashukuru kwa kuchangia nadhani hakuna such kind of the bussiness ila kuna utapeli ambao huwa unapangwa na watu ili kuibia wengine!!!!!Thanks alot
 
Mercury hutumika katika kuunganisha vipande vidogo vya dhahabu (amalgamation?) na hii kuifanya kuhitajika sana. Wachimbaji wadogo ndio wengi wateja wa hii madini. Hivyo basi utaona kuwa kwenye machimbo ndiko soko liliko na hadithi yote ya utajiri hutoka huko!Nani katajirika-sijui kwa kweli. Kwa hiyo kuwa makini maana sasa watakwambia nenda jeshini ndo inapatikana -na wajeshi si unawajua?
 
Wengine utawasikia sijui KARABAI ya mkoloni,,mara sijui Gwara lenye picha ya Trekta..
Watu tu wanahangaika,,ila ukimuuliza nani katoka kwa hiyo deal,,,hakuna jawabu..
Upanga kuwa muangalifu...


Hizo biashara zote ni upuuzi. Watu hawataki kutafanya kazi ili wafanikiwe kwa jasho lao. Ndio maana wengi wamekimbilia ufisadi na ushirikina. Hawataki kusumbua akili zao.

Wakati niko Sekondari tuliambiwa rupia ya Mjerumani ni dili. Nilipoenda likizo kidogo tuue vikongwe kwa kuitafuta. Tulizunguka maeneo tofauti mengine mbali sana, mwendo wa zaidi ya masaa 10 kwa miguu. Tuliambulia patupu. Mwishowe ikaja dili ya coins fulani za Tz zilitoka kwenye miaka ya 1986/87. Nilinunua kibao nikampa mshikaji wangu akauze Tarime (mpakani na Kenya) wakati wa midterm. Aliporudi akanambia hakupata soko ila coins hakurudisha! Kwa hiyo haya mambo ni utapeli tu!
 


Nimesikia watu nwengi wametapeleliwa na watu wanaodai wanajihusisha na biashara hiyo. kwanza mnunuzi na muuzaji wakati mwengine huwa ni mtu mmoja au wanafahamiana, muuzaji baada ya kukunganisha na soko anataka malipo kwanza kabla ya wewe kuona bidhaa halafu ukishalipa pesa ambay wao wanaona ni nzuri kwao wanabadili namba na kutoweka. kuna utapeli sana kwenye hiyo biashara
 
hilo kweli lakini kila mtu atakua na mpango yake
na mm kwaida nafanya deal zangu in public places
e.g five stars hotel ,, na mm si mara ya kwanza kufanya deal
hii ,, lazima kabla ya kila kitu amani ipatikane in both sides
and that what we alwYs deal with
 
Hamna mnunuzi kutuka tz wote watajiri ni kutoka
u
UAE, SAUDIA,EYGPT,SOUTH AFRICA
hii zebaki hua wanatumia kwenye petrol,bom,
dhahabu,na mambo ya uganga , sasa in our side
hamna utapeli kama tume fanye test na vifa vyetu na imekua orignal basi muzaji mwenyewe atasema wapi tukitane but in one condition iwe in public alafu tutarudia kufanya test ili tuhakikishe kua hakubadilishwa alafu yeye anahakikisha hela yake kamili basi kila mtu anaondoka zake
mbona watu wengi tuu wanaijua ila sema ni ya siri na huwa hawasemi wametajirika vipi
 
fuatilia hii link:
en.m.wikipedia.org/wiki/Red_mercury
 
Usijidangaje achana na biashara hiyo utaishiwa kutapeliwa
 
Any way atakaye kua tayari contact me maanake
kuna watu bado wameghafilika na ndo vizuri
 
Mama yangu wee! Hili ni tapeli kubwa kabisa! Kuweni macho! Angalia hata kiswahili halijui!
 
Macho
huna haki kabisa kuniambia tapeli cause hunijui
na kweli mimi sijui kiswahili vizuri kwasababu mimi
si mtanzanis lakini nimejitahidi sanaa na all my
times nasafiri
it seems kweli nimekosa nilivo ingia hapa but
narudia tena mimi si tapeli na mwenye rizki atafiks
kwangu kataa kubali macho , na baada ya leo
sitajibu mtu ila kama anataka kujua kitu kuhusu red mecury
alafu please respect your self otherwise you will lose others
respect cause you cant insult someone you dont know
have a nice day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…