Hii ni dedication kwetu sisi wahenga

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Habari za jioni wana JF
Imetokea nikapata tafakari (reminisce) utamu wa maisha yetu ya kale. Pale ambapo ulikua unajiandaa kwenda shule asubuhi, kwa mbaali unasikia kipindi cha "mazungumzo baada ya habari" kikiendeshwa na Marehemu David Wakati.

Unachukua begi lako pamoja na ufagio wako wa chelewa mdogo mdogo mpaka shuleni. Unakutana na mchaka mchaka wenye nyimbo za kumponda adui nduli Idd Amini. Break ya saa nne unapata vipande vyako vya miogo na chachandu unashushia na maji ya bomba.

Mzaha wa darasani unaendelea mpaka kengele ya saa nane amabapo kinapigwa kipute cha mpira wa makaratasi au kitenesi au gozi magoli madogo au one touch mpaka mtakapo muuzi mwenye mpira basi game inaisha.

Straight home umechafuka kama zombie, unachezea vitasa kwa kuchelewa, kupoteza peni na kuchafuka. Baada ya drama zote hizo, una chill unapiga msosi huku ukisikiliza kipindi cha MIKINGAMO.
Wahenga wenzangu mtaongezea utamu
 
kweli mkuu..kama sio mihogo basi ni visheti na karanga za kukaanga..nimekuwa wa kwanza kwenye huu uzi sababu mzee josee haya hajayapitia
 
Historical Truth

We, the people born between *1950-1990* are the blessed ones...

We are the awesome people... Our life is a living proof.

While playing and riding rented bicycle, we never bothered to wear helmets. We played marbles, tabala, dodging, skipping ropes, Etc.

After school time we played until dusk but never watched the world (TV) by locking up ourselves in a room.

We played only with our real friends, not with www.com friends.

If we ever felt thirsty, we drank tap water or water from the stream . bottled water didn't exist.

We never got ill even after sharing the same juice or drink with four friends.

We didn't put on weight even after eating plate full of sweets, garri, yam, plantains. On special days (Xmas. New Year) we had rice and chicken.

Nothing happened to our feet even after roaming and kicking ball made of rags or rubber bare footed

We never used any health supplements to keep ourselves healthy.

We used to create our own toys, bamboos, carton and milk tins.

Our parents were not rich, and they never chased after money. They just searched for and gave only love.. not any worldly possession.

We never had mobile phones, DVDs, Play stations, X-Boxes, video games, personal computers, internet, instagrams, Facebook, but we had many good friends.

We used to visit our friend's home unannounced and enjoyed food with them. We never had to call them and ask for their parents permission to visit their home.

Loving people were near to us so our hearts and souls were happy. Hence we never required any insurance policy.

We might have been in Black and White photos but you find colourful memories in them

The Ultimate is that we are a unique and the most understanding generation, because we are the last generation that listened to their parents and also the first that have to listen to their children.

We are the last set of people to treck kilometers bare footed to school, and yet carry our children to school in cars or by drivers.

The last generation to enjoy free public school education but the first to pay to train children In private schools.

We had less homework in our days so we could help our parents in home duties but have to assist our kids in their homework who cannot assist parents or maids in home duties.

We are not special, but a LIMITED EDITION and ENDANGERED SPECIES. I am proud I belong to this noble generation.

Please feel free to share if you are one of us.
 
Unakuta darasa lina timu za wababe na wanyonge. mnyonge hapati namba kwenye timu za wababe na mbabe haruhusiwi kucheza kwenye timu za wanyonge.Akiingia tu mchezo unavunjika maana wababe wanafahamika kwa kuchezeana rafu mwanzo mwisho ni kuumizana tu miguu. Kero ni pale kengele ya kuingia madarasani itakapogongwa
 
Ukifaulu unaweza ukachinjiwa ng'ombe, nyakati za likizo ukirudi nyumbani mbuzi na kuku ni halali yako kula na wakati wa kurudi shuleni unaoondoka na package ya mbuzi au kuku.Familia nzima ilikuheshimu na kukutukuza kisa tu unasoma sekondari
 
Tulikunywa uji wa buruga na mafuta '' msaada kutoka serikali ya Marekani''
 
Umenikumbusha mbali sana muhenga.......
Siku zile Radio Tanzania Dar es salaam au kwa kifupi RTD kati ya miaka ya 70, 80 na 90 waliovuma katika Idhaa zake za Kiswahili na Kiingereza. Wakati huo radio zilizotumiaka alimaarufu kama redio za phillps na national na panasonic na Nationalpanasonic (National na National panasonic ni kitu kimoja) au maarufu kwa jina la dudu proof

Orodha ya Majina haya hapa:

1: Abdallah Iddrissa Majura–Michezo
2: Abdallah Mlawa—Kijaruba, Ombi lako
3: Abdul Ngarawa -Taarifa ya Habari na Mazungumzo baada ya habari
4: Abisai Steven /Abou Liongo–Michezo
5: Ahmed Jongo–(Mpira, na mnazi wa kutupwa wa yeboyebo)
6: Ahmed Kipozi–Mpira
7: Alex Malumwene/Aloycea Maneno- Ombi lako, cheichei Shangazi, mama na mwana
8: Ananilea Nkya - Twende na Wakati, Jinsia, Utawala bora, Harakati

Nihao tu ndio ninao wakumbuka kwasasa
 
Kwenye nyimbo za mchakamchaka umenikumbusha kituko cha wanafunzi wa sekondari moja hapa jirani wanakimbia mchakamchaka kwa nyimbo za ajabu ajabu kama 'Oyooo Oyooo' na 'Mwanaume Mashine'.
anakazia mwanaume c wembamba mwanaume c kibonge........mwanaume mashine[emoji3] [emoji3] [emoji3] sekondar ya apa jilani ni rahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi hizo miaka ya 70, kuna jamaa alivunja dirisha la shule akiwa kidato cha 3.
Leo nimemuona kwenye media akimuonyesha mkewake, na akalipa fedha kwaajili ya ukarabati wa dirisha lile pamoja na mengine yalio haribiwa na wanafunzi watukutu kama alivyokua yeye......[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
Ila simtaji kwa jina...[emoji23] [emoji23]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…