Hii ni dedication kwetu sisi wahenga

nikirudi saa kumi nasaidia kazi za nymbani harakaharaka nikisubiri kipndi cha "KUTOKA AFRIKA" kilichokuwa kikielezea historia ya viongozi wa Afrika
 
Ahsante sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe hata wahenga wanaandika "Miogo" badala ya ''Mihogo?" nilidhani ni dot com tu wasiopenda kuitumia herufi H
 
Kipindi cha kijaluba na Abdala mlawa kwenye saa tatu usiku,
kipindi cha Philips usiku mida ya saa mbili hivi kama sikosei idhaa ya biashara,
kipindi cha sikiliza bwana umeme "kwa mwanga safi,mapishi bila moshi" Enzi hizo watu wengi tu walikua wakimudu kupikia majiko ya umeme hata uswahilini.
 
Halafu unamsikiliza Michael katembo na kipindi chake cha mbiu ya mikoa, yaani kwa mbwembwe nayeye alikua anaimba kwa kufuatiza ule wimbo wa kuanzishia kipindi,watangazaji Enzi hizo walifanya kazi kwa mapenzi na sio pesa tu!
 
Dah hakika umenikumbusha enzi ya kipindi cha "mama na mwana" RTD acha kabisa,yaani mkijua leo ndio kipindi na betri mpya hakuna basi za zamani zinaanikwa juani mapemaa haa haa
Kulikua na kipindi cha nenda kwa usalama barabarani
kikiongozwa na yule bibi Aloysia maneno, unaanza wimbo kabla ya kipindi..." Dereva kalewa gongo sawa hiyo? ataaa hiyo si sawa dereva acha vituko...."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…