Watanzania wenzangu kwa sasa tupo katika mchakato wa katiba mpya. Lakini kwa muono wangu nadhani katiba hii siyo ya watanzania kama tunavyotaraji. Katiba hii kwa sasa inatawaliwa na vyama vikuu viwili vya siasa yaani Chadema na CCM kupitia hii kitu wanayoita mabaraza ya katiba ya chadema au mabaraza ya CCM. Vyama hivi vimekuwa vikiwahubiria watanznia maoni ambayo yana maslahi kwa chama husika katika mikutano na vikao vyao, mwisho ndiyo hualika watu wachache kutoa maoni. Kwa hali hii inaandaliwa katiba ya ccm/cdm na siyo watanznia. Pia kumekuwa na kampeni ya kutuma maoni kupitia mabaraza mbalimbali ya vyama hivi. Swali ni je, maoni haya tunayoyatuma katika vyama hivi hayawezi kuchakachuliwa? Kuna teknolojia gani inayotumika, ambapo kama mtz nikituma pale ccm maoni yng yatafika pasipo kuchakachuliwa? Ilikuwa ni vyema Tume ikapita kwa watanzania na si haya mabaraza ya ccm/cdm. Mfano tazama suala la muungano, CCM wanataka serikali 2 kwa kutazama maslahi na kuwashawishi watu kukubali Chadema nao wanaamini serikali 3 ni daraja la kuwaweka Magogoni hivyo wamekuwa wakihubiri. Watanzania wenzangu tusikubali kuyumbishwa na wanasiasa tuangalie mambo yatakayotusaidia watu wa hali ya chini. Tuache kushabikia maoni ya vyama vya siasa yenye lengo la kubeba maslahi ya vyama vyao.