Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Nilham,
Kwa nini usiwe na raha siku ya birthday? Mie mwenzio tangia nilipofikisha miaka arobaini, nimeamua kila Ijumaa nifanye sherehe ya birthday. Kila mwaka ninakuwa na birthday parties angalau 52! Ukumbuke Nilham, furaha inakuongezea umri wako wa kuishi (other things remaining equal).
Ni vema kwamba unampenda mama yako, lakini nakushauri ukitaka furaha ya kweli wapende watu wote. Mie kwa mfano, nilimpenda sana mama yangu, lakini akafariki nikiwa na umri mdogo wa miaka 17. Hata hivyo namshukuru Mungu kwamba nimeweza kuishi na sasa nimeishi miaka mingi na walimwengu, ndugu na rafiki, zaidi ya niliyoishi na mama.
Birthday yako ni lini? Mungu akubariki.
Nilham unaweza kuwa unampenda sana mama yako ila unajihisi upweke cause unamiss kitu, labda mapenzi kutoka kwa umpendae wa rohoni yaan soulmate hii pi inawezekana.na hali inaweza kuwa hivyo hata kwa muhusika kutokujua ila ndio hivyo. embu angalia na hili pia.ni maoni tu
Jitahidi ifikapo siku yako kuzaliwa basi 'funga sunna', na ikibidi jitahidi siku 3 kabla ya birthday yako 'funga na zingatia ibada' kwa karibu saana. Hii ni ishara za shukrani njema kwa muumba wako.
LANGU: Katika hali za kiuchamungu...machozi huwa ni sehemu ya imaan ya mwaminio, zingatia.
Katika tamaduni za western China sherehe ya kuzaliwa uwa ni sawa sawa na msiba - Wao wanaamini kuwa unakaribia kufa (right?)...
Birthday inakuwa siku ya kukufariji ku-accept death!
Tatizo kubwa ni hilo (in red). Bila kujua sababu ya jambo, ni vigumu kupata ufumbuzi wake.
Kwa kweli, si kuwa sababu huijui sababu, bali usichokijua ni njia tu za kuifukua hiyo sababu. Moja ya njia hizo ni "kujitambua (self awareness)". Hili linahitaji maelezo marefu lkn ngoja nikushauri hivi: Kaa peke yako ktk sehemu ambayo kwako ni tulivu sana; ambayo hutapata bughudha yoyote -- vizuri ikiwa ni chumba kitupu au kisicho na samani (furniture) nyingi. Weka stool au kiti ktk kona mojawapo mbali nawe. Kisha mweke NILHAM ktk stool/kiti hicho. Sasa anza kumchunguza NILHAM kwa undani, historia yake tangu utotoni, maisha yake mtaani, shuleni, n.k., mambo anayoyapenda na asiyoyapenda; kwa kifupi, everything about her. Kubwa zaidi, chunguza udhaifu wake (huna la kuficha kwa sababu upo wewe, kivuli chako -- NILHAM in qn -- na Mwenyezi Mungu; wote hao hawawezi kutoa siri zako). Mtafiti pia NILHAM ili uweze kujua utatuzi wa kila tatizo na kikwazo. Ukiwa mkweli kwa NILHAM utajua mengi mno kumhusu yeye, na hivyo utajua pia njia za kutatua matatizo yake na kufukua uwezo na vipaji vyake.
Pole sana, hiyo ni hali inayowatokea watu wengi huenda ni ugonjwa!
Pole NR, kuna sehemu umesema kuna wakati unatamani umuombe mama msamaha kwa yote uliomkosea. Sio vibaya ukifanya hivo lakini sio lazima hiyo siku ya birthday. May be kuna uponyaji unaweza ukaupata kupitia hilo. Manake sisi watoto wa kike bwana kuna wakati unaweza ukakupitia ukajikuta unamdharau mama tu bila sababu ya msingi......lakini unapopata akili za kiutu uzima unajikuta unajutia.
Halafu naomba usimbebe sana mama moyoni, sina maana usimpende hapana, mpende mama, masaidie, mjali lakini kumbuka pia huyo sio mali yako ni mali ya Mungu pia. Kwa sababu ukimbeba sana moyoni siku mwenye naye akimchukua (MUNGU) utaumia zaidi na utakuwa na majeraha ya moyo yasiopona mapema.
Be blessed NH!!!
Dah!
Pole nilham.
Mi pia nina tatizo kama lako ila sio kwenye birthday.