Hii ni kwa wana VICOBA au mwenye mke, mume au ndugu aliye kwenye VICOBA

Hii ni kwa wana VICOBA au mwenye mke, mume au ndugu aliye kwenye VICOBA

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Idea ya VICOBA ambayo ilianzia India miaka ya 80 huko ilikuwa na lengo kuu moja kwa ajili ya kuhakikisha wale walio tengwa na taasisi lasimi za kifedha wanafikiwa.

Financial Inclusion. Kuhakikisha wote wanafikiwa hasa waishioa vijijini. Haikuitwa VICOBA kwa bahati mbaya.

Miaka ya 90 VICOBA au VSLA iliingia Africa hasa kule Niger na miaka ya 2000 ndo iliingia Tanzania ila ilitestiwa kwanza kule Zanzibar kuna sababu. Na baadae ndo ikaenea Tanzania bara.

VICOBA
Hivi vikundi ili vifanikiwe kuna mambo kadhaa na mki mess kimoja tu inakula kwenu.
1. VICOBA lazima iundwe na watu wanao fahamiana kitabia- Hii haina mbadala.

2. VICOBA lazima itawaliwe na wanachama wenye upendo miongoni mwao-Upendo ndo nguzo kuu ya VICOBA.

3. VICOBA lazima wanachama wote wawe wanakutana sio wanatumana pesa hapana wanakutana- Hapa ndo loop holes ya upigaji VICOBA ulipo. Make kikundi cha watu 30 wanakutanaga watu 14 tu wengine wote wanatumanaga tu pesa hapa ndo upigaji mkuu ulipo.

4. VICOBA wanachama lazima sio tu kuhamaiana bali kujuana uwezo wa kila mmoja. Kwamba fulani ana uwezo fulani na fulani ana uwezo fulani.

5. VICOBA sio kwa matajili au Middle class, matajiri wakakope Benki, hawa ndo wanao haribu VICOBA, ukipna mtu ni takiri yuko likoba basi jua kifuatacho ATV ni upigaji tu.

6. VICOBA ni kwa watu wote wa levo moja, sio wengine wana pesa sana wengine hawana kitu kabisa. Hapana wote wawe levo moja ya maisha.

7.VICOBA ni daraja la watu kupita na kwenda sasa kukopa taasisi kubwa, Idea ya VICOBA ni kuwajengea watu nidhamu na Confidence ili baadae wakakope taasisi kubwa.

8. Msiache VICOBA ikakua kupitiliza- Hapa ndo hata yale mambo ya kule Arusha yalitokea,Milion 39 zitawekwaje kwenye sanduku ndani?
VICOBA ikionekana inakuwa basi inadilini kuwa SACCOS,

9. Ukuaji wa VICOBA ni kubadilika kwake kuwa SACCOS na sio kuwa na pesa nyingi.

10. Kwa Techinolonia ya sasa. Chonde Chonde Chonde Chonde chonde chonde Pesa zihifadhiwe Benki, jamani narudia na kurudia pesa zihifadhiwe Benki.

11. Kwa techinolojia ya saaa Chonde chonde wanachama wote wawe na Account benki, wawe na Account benki ambayo ndo inahifadhi pesa zao.

12. Kwa mazingira ya sasa Mkopo wa mwanchama akapewe benki yaani pesa itoke kwenye account ya kikundi iingie kwenye account ya mwanachama. MUHIMU SANA HII.

13. Kwa mazingira ya sasa CHONDE CHONDE CHONDE CHONDE CHONDE CHONDE kwenye kugawana pesa mHesabu yapigwe yapelekwe benki na benki ndo iwaingizie kila mtu kwenye account yake.

14. Msiruhusu ujanja ujanja kwenye kikundi hata siku 1.

15. Kila wiki wanachama wapewe taarifa ya makusanyo hata kwa sms hiyo iwe ni razima na sio ombi.

16. Pesa ambazo hazikopwi zipelekwe benki.

17. Kama ndani ya kikundi hamjuani hata fulani anakaa wapi na anafanya nini hii ni hatari tupu.

Kuna upigani mkuy VICOBA kwa sababu kuna loop holes za kufa mtu na kuna wajanja.

MWISHO

Upendo usipo kuwepo basi uipigaji huiingia, tamaa, kutaka kutajirika kupitia michanho ya wanachama.

VICOBA upigaji ni yale yale yalio kuwa yanafanyika kwenye Ushirika, kilicho ua Ushirika ndo hicho hicho kiko kwenye VICOBA, tamaaa kuu ya watu.


By
Chasha
 
Back
Top Bottom