Hii ni kwa Wanaohusika na taaluma ya Ujenzi wa Nyumba

Hii ni kwa Wanaohusika na taaluma ya Ujenzi wa Nyumba

A3M

Member
Joined
Jul 23, 2019
Posts
84
Reaction score
178
Habari Wana JF.

Ni matumaini yangu mko poa na mnaendelea vizuri na Shughuli za Ujenzi wa Taifa. Wakuu Mimi naishi nje ya nchi na sitarajii kurudi kwa miaka hii mitano inayokuja lakini nahitaji kujenga Nyumba ambapo kiwanja kipo tayari nilishanunua ila tatizo sina mtu wa kunisimamia.

Hivyo naomba kujua kampuni inayoaminika inayoweza kunifanyia Usanifu, Manunuzi na Ujenzi ili tuweze kufanya kazi maana sina ndugu ambae namuamini wa kusimamia Ujenzi wangu hivyo nahitaji Kampuni ya Uhakika ya kufanya nayo kazi.
 
Mzee huko ni kujitengenezea mazingira kupigwa...na kukaa kwote ,ughaibuni unawaza Jenga..nenda nssf.utumishi nhc wana appàrtment kibao bei za kizalendo
 
Unajenga kwa ajili ya nani?,Nyumba si ni yako?kama huamini mtu tulia huko mpaka utakaporudi ujenge na usimamie mwenyewe.Ukiwa na hela siku 40 unamaliza nyumba na kuhamia.
Kweli Kaka?
 
Unajenga kwa ajili ya nani?,Nyumba si ni yako?kama huamini mtu tulia huko mpaka utakaporudi ujenge na usimamie mwenyewe.Ukiwa na hela siku 40 unamaliza nyumba na kuhamia.
Siku 40 unamalizaje ujenzi
 
Unajenga kwa ajili ya nani?,Nyumba si ni yako?kama huamini mtu tulia huko mpaka utakaporudi ujenge na usimamie mwenyewe.Ukiwa na hela siku 40 unamaliza nyumba na kuhamia.
Najenga kwaajili yangu
 
Habari Wana JF,Ni matumaini yangu mko poa na mnaendelea vizuri na Shughuli za Ujenzi wa Taifa.
Wakuu Mimi naishi nje ya nchi na sitarajii kurudi kwa miaka hii mitano inayokuja lakini nahitaji kujenga Nyumba ambapo kiwanja kipo tayari nilishanunua ila tatizo sina mtu wa kunisimamia hivyo naomba kujua kampuni inayoaminika inayoweza kunifanyia Usanifu,Manunuzi na Ujenzi ili tuweze kufanya kazi maana sina ndugu ambae namuamini wa kusimamia Ujenzi wangu hivyo nahitaji Kampuni ya Uhakika ya kufanya nayo kazi
Acha uboya mkuu, kama unashindwa kumuamini ndg yako nani mwingine utamuamini?

Nakushauri, tafuta hiyo kampuni wakupe gharama zao na kila kitu then ndg yako ndie awe anasimamia ili kuendana na gharama pamoja na ubora.

Wakishajua haurudi siku za katibuni watajenga na utamuambia ndg yako akakague na atakuta kweli kuna nyumba lakini kama ni ya kiwango cha chini basi within 3 yrs kinakuwa kifusi tu.
 
Ukikosa humu

Watafute FREEMASON ,Wajenzi huru watakujengea kila kitu
 
Back
Top Bottom