Hakuna anaewapangia matumizi ya pesa zenu. Lakini ninaomba kuuliza, ni lazima mkifika bar au pub mnywe mpaka mlewe?
Kunywa bia moja au mbili ni nzuri kwa afya hasa baada ya kuuchosha mwili siku nzima. Lakini mara nyingi watu wakusanyikapo bar hunywa bia tano kuendelea.
Ninaomba radhi kwa kuwaharibia sukukuu lakini mkumbuke pombe husundikwa na sukari. Hizo calories mnazilundika kila siku mara nyingi huishia kwenye hypertension na diabetes.