Ingawa viwanda vya sigara huambatanisha kemikali nyingi katika utengenezaji sigara, lakini muhimu kuliko yote ni kemikali hii iitwayo "Nicotiana tabacum" , kemikali hutokana na majani ya tumbaku na ndio inayomfanya mvutaji awe na kiu ya sigara kila mara.Kiasili kemikali ya "nicotine" ni kichangamsho, kichocheo au kiburudisho. Kwa sababu hiyo basi ndio maana wavutaji wengi wakiwa kwenye msongo, mfadhaiko au hasira hukimbilia kuvuta sigara ili walau munkari utulie.