Hii ni misemo ambayo inamrahisishia shetani kazi yake

Hii ni misemo ambayo inamrahisishia shetani kazi yake

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Kimsingi shetani yuko smart sana kiasi kwamba kumzidi ni ngumu. Hutumia binadamu wenyewe kufanikisha mambo yake.

1. "Fuata ninachosema usifuate matendo yangu"
Hii mara nyingi ni kisingizio kinachotolewa na baadhi ya viongozi wa dini au watu wengine waliojipambanua kama wenye maadili bora.

2. "Mungu anaangalia rohoni na sio mavazi"
Hiki ni kisingizio kikubwa miongoni mwa wakristo wengi wakitetea uvaaji wa kihuni makanisani.

3. "Siwezi kuingilia faragha ya mtu, ushoga ni suala la faragha"
Hii kauli maarufu sana toka kwa makada wa chama kikuu cha upinzani na watetezi wengine wa haki za mashoga.

4. "Wezi wa mali za umma kwenye ripoti ya CAG wameachwa halafu wezi wa kuku ndo wanahukumiwa"
Hii kauli ya kipumbavu hutamkwa na watetezi wa wavunja sheria kwa kisingizio cha kutohukumiwa kwa waliotajwa kwenye ripoti ya CAG. Cha kushangaza wao wakimkamata mwizi humchoma moto hadharani bila kumfikisha mahakamani.
 
Back
Top Bottom