Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Jana ilikuwa siku maalumu ya baba yetu wa taifa hili. Niliitumia kutafakari maneno yaliyosemwa na Roma kwenye wimbo wake kuwa Tanzania ni nchi iliyobeba udongo wa dhambi ila tunalisaka sana taji la ushindi.
Ni maneno yenye tafakuri pana. Mlimwengu mimi napata picha halisi wakati tukiwa katika kipindi hiki cha kutafuta viongozi wa taifa hili. Nikirejea kwenye maandishi ya Mwl Nyerere kwenye kitabu chake cha Ujamaa (1977) alisisitiza maendeleo yatatokana na vitu vinne ambavyo ni siasa safi, watu, ardhi na uongozi bora.
Ninapoangalia kwenye kipengele cha Siasa safi na uongozi bora namuona baba yetu mwenye maono Dr John Magufuli anavyovivaa viatu vya mwasisi wetu. Wazalendo wote tarehe 28 tutaenda kupiga kura za kutosha kwa Rais wetu Dr Magufuli kwa sababu ya kulinda amani na usalama wa nchi yetu. Hili ni taifa la watanzania na litaongozwa na watu wenye vinasaba vya kitanzania siyo vibaraka ambao wanatumwa na mabeberu.
Hii ni nchi yetu na watakaoamua hatima ya nchi yetu ni Watanzania. Hatutakubali watu wenye sura mbili mbili kuwapa madaraka ya nchi hii. Wazee wetu walipigana kutafuta huu uhuru. Mtwa Mkwawa akisikia tunataka tuwarudishie atajisikiaje? Je, Kinjekitile atapata picha gani? Mwl Nyerere kapumzika pale Butiama nadhani hata kaburi litapata mtikisiko kukubali nchi yetu kuirudisha kwa vibaraka wa mabeberu.
Leo hii Tanzania ni moja hatuna ukabila; Mzaramo na Msukuma wanakaa pamoja, Mmasai na Mhaya wanaoana. Tunaunganishwa na utanzania na lugha yetu ni moja ambayo ni Kiswahili.
15/10/2020
Mo Mlimwengu
mohammedismail613@gmail.com
Mlimwengu mimi nawatakia tafakuri njema.
#mlimwengumimi