Hii ni sahihi kweli?

Mundu Lunda

Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
32
Reaction score
2
Mimi ni mwalimu serikalini tangu 01.03.2013, mwaka huu mwezi wa nne mapema tu niliomba likizo ya malipo ili niende wa sita wakati wa likizo, na hii ni kutokana na sheria za utumishi wa umma kama zinavyojieleza kwenye 'standing order' ambapo inasema mtumishi ana haki ya kuomba likizo ya malipo kwa mwajiri wake baada ya miezi 8 tangu kuanza kazi.
Sasa jana nimekwenda halmashauri nikakuta tangazo linasema "wafuatao waje wachukue fedha zao za likizo" na jina langu likiwemo nami bla kuchelewa nikaenda ofisi ya fedha ili nipewe changu, nkaambiwa pesa yako ipo nenda kalete kibali toka kwa mkuu wako wa idara ili nije nikupe pesa yako, lakini sasa cha kushangaza nilipokwenda kwa viongoz wa idara yani DEO na SLO wakadai ya kuwa sina sifa ya kupewa hiyo pesa ya likizo eti kwa sababu bado sijatimiza muda wa kupewa likizo ya malipo.

Hiki ndicho hasa kilichonifanya niandike huu uzi hapa kwa ndugu zangu wa JF nikiamini wazi kabsa hapa kuna wataalamu zaid wa haya mambo na watanisaidia. Karibuni kwa mawazo wandugu.
 
labda ungewauliza wao wanataka sifa zipi ambazo wewe hauna?,na kama ulikuwa hauna sifa kwanin wakuweke kwenye orodha ya malipo?,na kama hukuwa na sifa walikupaje ruhusa ya kwenda likizo?,inakuwaje ukose sifa halafu hela yako ya likizo iwepo?.Mdau ngoja na mim nisubir wataalam waje watujuze
 

kiukweli haya mambo yanashangaza sana ndugu, mana hata ukiwahoji majibu ya kuridhisha hawana, waliyonayo ni ya kukela tu.
 
Kwa uelewa wangu mdogo Wa utumishi ni kuwa likizo ya kwanza unachukua bila Malipo mwaka unaofuatia unalipwa na hii ni endelevu mwaka huu unalipwa unaofuatia ni bila malipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…