Hii ni stori ya maisha yangu. Nini ushauri wako kwangu?

mkuu kwenye maelezo yangu hayo nilivyoelezea ni mapito yangu ili kufikia lengo lakini nimeona mengi nimeyafanya ambayo si kipawa hivyo inapotokea changamoto navumilia kwa kadri na kama hakuna matokeo chanya naachana hiyo naanza kingine ,kwa imani yangu na kwa kuwa tayari nilijaribu kwa muda wa miaka 2 ufundi badhii ya mapungufu niliyoyaona na changamoto nilizo ziona basi ilinilazimu niweze kutafuta education ya hiyo kitu na ndo naenda miezi hii kupiga shoti course ya phone repair si hvyo tu pia excess cash ambayo itaniwezesha kufanya uwekezaji mzuri kabisa kwa kununua materials yate yatayohitajika napo anza lakini huku kwa kazi yangu wakati huu nimeiboresha hvyo kwa sasa hainitegemei mimi kuwepo kazini ndo iende kiasi flani nina uhuru wa muda wangu,hivyo naweza kulifanya kwa awamu nyingine tena hilo jambo.
 
Kitu kibaya katika maisha ya mwanadamu ni kutokujua na kutotambua anachokitaka.
Sababu ataishia kuhangaika huku na huku pia kuendeshwa na mitazamo na mawazo ya watu milele bila ya mafanikio.

Mtu asiyejua anachokitaka na kukitafuta ni kama kipofu aliyepotea njia ila anaendelea kwenda tu.
Na siku huyo kipofu anakuja kushtuka atajikuta yupo mwisho wa reli lakini hajui wapi alipo.

You see mkuu, maana ya mafanikio zinatofautiana kati ya mtu na mtu.
Kwa maana hiyo basi ni wazi na bila shaka njia za mafanikio lazima zitofautiane kati ya mtu na mtu.

Sasa kama wewe unaona fulani amefanikiwa kwa kilimo, afya, ufundi alafu na wewe unafanya hicho'hicho ili ufanikiwe basi ni lazima utakuwa hujui unachokitaka na kukitafuta maishani mwako.

Na hapo ndipo tatizo lako lilipo mleta mada.

Kila mtu ana maana yake ya mafanikio lakini njia ya kila mtu kufika huko anapopataka ni moja tu.
Mafanikio ni matokeo ya hardwork, juhudi binafsi, kujielewa, kujitambua na kujiamini pia kuwa na mipango mikakati , clear plans and goals.
Kuwa na Short term plans/goals na Long term plans/goals.

Ili upate mafanikio ni lazima uwe unajua unachokitaka na kukitafuta then uwekeze nguvu zako zote hapo no matter what happens wewe utaendelea kuweka nguvu, focus, maximum efforts mpaka kieleweke au mpaka unakufa hakuna kuquit until you drop dead.

Na kitu cha muhimu katika kujua unachokitaka maishani na kufocus kwenye jambo moja na kulipigania ni kwamba utakuwa na uzoefu nalo wa kutosha hivyo utajifunza mengi na kujua insides and outs kiasi kwamba hata ukidondoka automatically utajua jinsi ya kusimama bila kupoteza muda.
Kuliko kuranda'randa huku na huku then unatoka empty.

Pia mkuu nimenotice kitu kimoja kutoka kwako hivyo nakupa ushauri wa mwisho huu hapa!

Na msingi wa yote katika niliyoyaandika hapo ni kutambua kwamba katika maisha hakuna kitu rahisi.
na kama vipo vitu rahisi basi jua vimegharamiwa na kuhangaikiwa kwa jasho hivyo gharama yake ni kubwa na siku zote mwisho wake ni mbaya.
 
Jaribu na kifuga kuku nasikia Kuna utajiri huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo chai TZ hakuna Bachelor ya Plambing, Electrical, Ujenzi ni kwa pamoja hii ni chai mbichi ambayo haina majani wala iliki au tangawizi
 
Wacha nikushauri mkuu mi naona katika hayo yote uliyoyafanya hakuna linalokufaa ila unayaweza yote, wewe inaonekana ujaumbwa kufanya kazi , wewe umeumbwa kusimamia kazi ndomana unapenda kugusa kila jambo, sasa cha kufanya fanya yote ila anza na kimoja kimoja, mfano hapo unafanya labs then unafunga ofisi ya ufundi unamweka kijana anamfanyia management unahakikisha anapita kwenye njia yako, ila huyo kijana usimfanye umemwajili bali afanye awe ni partner wako jipe muda kidogo hapo pakiweza kijiendesha, achana napo weka partner mwingine hapo labs kisha achana napo tafuta project nyingine tena, wewe ni manager tu take it from me, managers wengi wanacharacter km zako, unamkuta anacertificate kibao na anapenda kujifunza kila siku na kujaribu jambo jipya..
 

Kila kitu yeye....halafu anakata tamaa mapema
 
Ushauri makini huu.
 
ni sahihi ulichokinena kwa asilimia nearly 100 kwani kwanza tangu nijifunze kozi karibia tatu japo nyingine sjaziweka,hata sku moja sjawahi kutamani kufanya applications ili niweze ajiriwa japo mwanzo niliwahi kujishikiza sehemu kwa ajiri ya kupata captal ,kila sehemu nilipo utanikuta nimeanzisha zaidi ya kitu kimoja kwa mfano eneo nilipo sasa nina pub,hapo nina restaurent hivyo hivyo duka la dawa na medical lab.nimefanya decentralization ya management. pub yupo kijana na bar meds,resta anasimamia mke akiwa wasichana wa kazi na duka la dawa nipo mimi na kijana wa duka la dawa lakini pia lab technician mmoja ambaye amejiegesha hapa karibia 6monthes hivyo ndo nataka awe pamanent .kutokana na ushauri wako kweli mimi najiona kama project planner and manager .
 
Mkuu,kujua vitu vingi ni jambo zuri ila kufanya vitu vingi ni ujinga hasa iwapo haviingiliani au kupeana support.Kwa mfano ukiwa mtaalamu wa maabara halafu ukafahamu kuhusu tiba asilia unaweza kuwa tabibu mzuri.Ukiwa mkulima wa mazao na ukawa pia mnunuaji na muuaji ni jambozuri pia.Ukiwa fundi redio pia nijambo zuri.

Swali ni JE what is your end game?What is your game plan?
 
[emoji16][emoji16]jmn ktk kuhangaika si unajua tena!
 
Fanya ufanyavyo,chagua kimoja unachokisikia ndani!
Lkn ili ufanikishe bila Mungu (Yesu)utaishia kuhangaika,muweke Mungu kwanza ,omba ulinzi wake sio kwenda kwa watu wa Tiba asili huko labda wasiwe waganga!

Sababu nimesoma btw the lines naona km kila unapoanza kufanikiwa unaugua,kuumwa kupata tatizo!
Haijakaa sawa hii! Ss km umewekewa mipaka ya kutofanikiwa hata ufanye unachokipenda lzm utaishia kuhangaika ,mtafute Mungu bro!

Haya mambo yapo.
 
Kiufupi umerogwa haujielewi
Kabisa,hayuko sawa.
Yaani hii ngoma ikienda kwenye deliverance utashangaa!

Huyu kawekewa mipaka hakuna kutoboa,ndo maana anahangaika akitaka kutoboa anaumwa,ulimwengu wa roho wa ajabu sn,uko makini kuhakikisha unasimamia kilichonenwa ili kitimie!
 
Nimesoma andiko lako la hii makala kiukweli unajitahidi sana kupambania future yako ya maisha lakini unachoambulia ni kiduchu sana,nataka nikuambie hasa niende kwenye mambo ya kiroho yaani ulimwengu wa roho,kuna nguvu kubwa inapambana na ww usifanikiwe na hata ukifanikiwa ni kiduchu mno, hiyo nguvu ipo kwenye ulimwengu wa roho ambao umegawanyika nuru na giza ,ww nguvu hio ni giza inapambana usiende kwenye nuru ambayo ni mafanikio ya mwanadamu ndo yalipo ,maana ya ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao kila jambo linafanyika pasipo kuonekana,mimi ushauri tafuta haya makanisa binafsi mfano mwamposa ,mwingira,mzee wa upako,nakwambia utakuja nishukuru kwa ushauri wangu
 
Angalia kipi unakipenda na kina maslahi jifue kisha ingia mazima, upambane. Ukiwa mbobevu wa kile unachokifanya kitakutoa tu haijalishi ni kitu gani.

Suala la afya nadhani ni kufanya vipimo zaidi kujua tatizo lipo wapi.
 
Umekosea kuquote mkuu, mwenye uzi ni mbuyake sio mimi.
 
Pia mwombe Mungu akusimamie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…