Nilitamani sana kuoa Mchaga but nasikitika Mmachame niliyempata mimi sijui alikuwa wa wapi.....!!! Alikuwa akija kwangu, sikatai kwenda kwa mpenzi ni sehemu ya mapumziko lakini huyu alikuwa kiboko!!
Asubuhi alitaka nimpeke kwa hotel kupata break fast then nimrudishe home! Mchana nikamchuke nimpeleke luch then nimrudishe home, jioni vile vile daaah alikuwa anaangalia TV huyo mpaka TV inamuonea aibu!!! Nilidhani ata-change lakini ikawa ndiyo hivyo hata akae miezi miwili kwangu, na ndani nilikuwa na kila kitu tena vya kurahisisha mapishi hata kwa wananume kama vile jiko la gas, pressure cooker, deep fryer, rice cooker, etc.
Nilijitahidi kumbadilisha lakini hakubadilika nikaamua kumwagiliako mbali tena nikimpa live sababu za kumwaga ingawa nilikuja kugundua kuwa hajui kupika kabisaa so ilikuwa ni kama kumuonea vile but ndo hivyo hakuwa wife material!!! Ni kosa la familia yake naamini!!!
Nikajikuta nahamia pande za Pareni!!!