Hii ni Taifa Stars iliyoifunga Zambia kuingia African Cup (Tumemkumbuka Peter Tino, tumemsahau Thuwein Ally)

Wachezaji wa zamani wanapaswa kuwa na umoja wenye nguvu sio kuishia kujisifia enzi zao walifanya nini.
Mbwana Samatta ni mchezaji aliyefanikiwa kuliko wote katika historia ya Tanzania lakini humsikii akiongea au kufanya jambo pasipo akili ya ziada.

Pale ikulu leo mchana walitakiwa wawepo wachezaji wengi kuliko hawa wauza sura wa kibongo tunawaona kwenye runinga mara kwa mara. Lakini alikuwepo Tenga na TIno.

Pengine wingi wa wachezaji wa zamani ungeweza kumfikirisha rais JPM akaweza kuja na wazo jingine lenye faida kwa wanasoka wote wa zamani.

Kumlaumu au kumsema vibaya Tino hakuna msaada wowote, kakabidhiwa kiwanja na kapewa milioni tano kwa sababu alikuwepo mle ukumbini.

Wachezaji wa zamani wengi wao kwa bahati mbaya elimu ndogo, wanakosa nguvu ya ushawishi, tofauti na wachezaji wa zamani wa Zambia, Nigeria na mataifa mengine yenye kutambua nini maana ya elimu.

Nafasi ile ile aliyopewa Tino kuongea mbele ya watu na rais JPM angepewa Segun Adegbami au Okocha au Kalusha Bwalya angeongea mambo ya msingi ndani ya dakika chache alizopewa.
 
Umeachanganya mambo. Kajole aliondolewa mechi na Zambia, Qualifying match, ya mwaka 1979. Mechi ya Segun ilikuwa ni March 1980 kwenye finals pale Sururere.

..OK.

..lakini unakumbuka mechi tuliyocheza na Nigeria Surulele?

..unakumbuka goli la kwanza lilitokea upande gani? Lilifungwa na nani? Na ilikuwa dakika ya ngapi?

..ninachokumbuka ni Segun Odegbami kutawala mchezo ndiyo maana nikasema huenda Kajole alikuwa substituted.
 

Kwenye hiyo picha ya Taifa Stars, Kutoka kushoto ni:

Godian Mapango (Pan), Salim Amir (Balimi-Bukoba), Idi Pazi (African Sports), George Kulagwa (Simba), Thuwein Ally (Simba), Ibrahim Kiswabi (Pan), Peter Tino (African Sports), Omar Hussein (Yanga), Juma Mkambi (Yanga), Hussein Ngulungu (Pan), Juma Matokeo (Pan), Mohamed Salim (Coastal), Adolf Rishard (Pan).

Uwanja wa Ndege ni Dar Esalaam International Airport, Terminal 1
 

Hoja yangu ambayo umeikiri ni kwamba Segun ni mnigeria aliyekutana na Taifa Stars March 1980 wakati wewe ulikuwa unatuchanganya kwamba Kajole aliondolewa akaletwa Amasha wakati kitendo hicho kilfanyika Zambia mwaka 1979.

Hayo mengine unayoyaleta siyo hoja yangu.
 
Asante mkuu kwa kumbukumbu nzuri. Segun aliwatesa sana kina Tenga.
 

Usichanganye kama wenzako. Ni kweli mwaka 1979 na hata 1980 African Sports alikokuwa Peter Tino ilikuwa haijapanda daraja.

Lakini mwaka 1979 na mwaka 1980, Peter Tino hakuwa Pan alikuwa bado African Sports. Peter Tino ameingia Pan mwaka 1981.
 
Hivi hizi stori za kuwa Kajole alikuwa anakimbia hadi anauacha mpira nyuma ni za kweli au kahawa tu??

Sent using Jamii Forums mobile app

Aliyekuwa anakimbia na kuuacha mpira nyuma alikuwa ni winga Sunday Juma wa Simba. Kajole alikuwa na sifa ya kupiga kona inaingia golini yenyewe, tena kwa mguu wa kushoto.
 

..hakuna anayemsema vibaya au kumlaumu Peter Tino.

..wa kulaumiwa ni hawa wanaopotosha historia ya soka la Tanzania.

..Wizara ya Michezo, chama cha mpira, na Ikulu, ndiyo waliotuangusha
 

..Hussein Ngulungu hakuwa Tumbaku ya Moro?

..Na Salim Amir hakuwa Coastal Union ya Tanga?


..hebu rejea kavazi[ archive] yako halafu utupe mrejesho.
 
Umeandika vyema Sana

Hussein Ngulungu ndie aliempa Pasi Pater Tino

Rais kumpa zawadi Peter Tino Ni sahihi na itaendelea Kuwa Sahihi

Rais katoa zawadi kwa mfungaji wa Bao lililotupeleka Nigeria hakusema Kuwa zawadi ya Man of the Match!

Una kumbukumbu njema Sana Wanyamwezi wanaita 'Photographic memory' Yaan hujaacha kitu
 
Aliyekuwa anakimbia na kuuacha mpira nyuma alikuwa ni winga Sunday Juma wa Simba. Kajole alikuwa na sifa ya kupiga kona inaingia golini yenyewe, tena kwa mguu wa kushoto.
Huyo alikuwa anaitwa Willy Mwaijibe "Winga Tereza"
 
Jamaa alikuwa ni mzuri sana katikati ya dimba, nakumbuka walivyokuwa wakigombea namba na Roma Mapunda pale Pan Africa. Lakini ili kuweka kumbukizi sawia na kuondoa upendeleo, ni vyema tukawapa hadhi wale wooote waliohusika katika kuipeleka Stars Lagos 1980. Hii ya kuleta kumbukizi ya mchezaji mmojammoja haipendezi, ile ilikuwa ni timu na ilikuwa na watu wengi na kila mmoja alikuwa na mchango wake kwa nafasi yake aliyotumikia.
 
Mbona hili ni la kutumia akili ndogo tu kuelewa? Swali aliyetupeleka African Cup alikuwa ni Nani?

Inawezekana Huyo Thuwein Ally alifunga hayo magoli....lakini bahati mbaya hayakuwa na msaada kwa team maana mwishoni tulitolewa. Nampongeza pia kwa juhudi zake. Ila asingepata nafasi ya kufunga huko mama PETER TINO ASINGEFUNGA LILE MOJA KULE ZAMBIA

PETER TINO HOYEEEE !
 
Wakati tukifikiria kuwaenzi wachezaji wetu wa enzi... Pia tuwape HESHIMA yao waliojitolea kuweka hz Historia za zamani!

Pale Morogoro, jirani na Shule ya Msingi MWEMBESONGO ndio palikuwa Nyumbani kwa akina JELA MTAGWA!

Binafsi nimetumia POSTA STAMP zilizokuwa na Picha ya huyu Guru! Tukiwa wadogo pale Morogoro.
 

..Tulicheza mechi ya kwanza Dsm na aliyefunga goli alikuwa Mohamed Rishard "Adolf."

..Jiulize kwanini tulifuzu kwenda Lagos kwa matokeo ya bao moja kwa moja.

..Mohamed Rishard naye anastahili sifa sawasawa na Peter Tino.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…