Hii ni Tanzania. Ishi ukiwa na akili zako

Hii ni Tanzania. Ishi ukiwa na akili zako

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
1. Karibu bongo ambapo watu wapo bize na habari za maisha ya wasanii kuliko kufuatilia afya yake.🤗

2. Karibu bongo ambapo harusini lazima lipikwe pilau.🙄

3. Karibu bongo ambapo mtu ana funguo ya gari hana gari.🤔

4. Karibu bongo ambako ni rahisi kwa jamaa zako kuchangia pesa kwa ajili ya kuharibu maini na kutoa rambi rambi za maziko yako lakini ni vigumu kupata pesa za kukusaidia kuanzisha biashara.🤐

5. Karibu bongo ambapo watu wanaamini kila alietoka nje ya nchi ni tajiri ata kama umetoka Sudani.🙁

6. Karibu bongo ambapo mtu anajiunga bando la wiki kila siku.😓

7. Karibu bongo. Nchi ambayo mwanaume aliyeoa bado atalalamika kwamba mchepuko wake unamsaliti.🤕

8. Karibu bongo ambapo vinyozi wanaonyesha picha za staili hawawezi hata kuzinyoa!😬 Ukimuona anatazama sana kioo ujue tayari ameharibu kazi.

9. Karibu bongo ambapo watu watalalamika kuongezeka kwa bei ya bando lakini watakaa kimya bei ya sukari na unga ikiongezeka.👀

10. Karibu bongo ambapo mtoto anapewa jina la kizungu pasipo kufahamu historia ya jina husika.😂

11. Karibu bongo ambapo dawa moja huponya magonjwa yote hasa ukisema inatibu nguvu za kiume Ndio utauza fasta😠 Wamasai kula chuma hicho.

12. Karibuni bongo ambapo mwanamke mwenye matackle na maziwa makubwa anajiamini kuliko mwanamke msomi mwenye shahada.

13. Karibu bongo ambapo wavulana hutembea na wanawake wenye umri mkubwa (mishangazi) na mabinti hutembea na Mababu hao huitwa masponsa.😇

14. Karibu bongo ambapo watu wanaamini ukiwa na gari umetoboa kimaisha hata kama la mkopo.🤗

15. Karibu bongo ambapo michezo ya kubet imekuwa ajira kwa vijana.🙄 Na inaingiza pesa ndefu sana katika mapato.

16. Karibu bongo ambapo kwenye familia za kawaida ukifeli o level unatafutiwa bodaboda au bajaji.🤔

17. Karibu bongo ambapo binti wa 2000 ni mkubwa kuliko mamake, elewa neno MKUBWA😎 Binti ana body count kubwa kuliko body count ya Mama ukijumlisha na Bibi yake.

18. Karibu bongo ambapo vijana wengi hawana ajira na wala hawataki kujiajiri ila wana ndoto za mafanikio..🙁

19. Karibu bongo ambapo mtu kama hauna connection hutoboi...ng'oo ata uwe na degree mbili. 😤

20. Karibu bongo.. Ukivaa kanzu kisha ukabeba chupa ya chai utaitwa muuza alkasus mujarab. 😤

22. Karibu bongo ambapo ukiwaona kwenye social media mabosi ukikutana nao live wanaomba hela za bando😠

23. Karibuni bongo ambapo wanaume waliolelewa na SIngle Mother na Baba wa Kambo hawataki kuoa Single Mother hawatai kuwa Baba wa kambo😤

24. Karibu bongo ambapo tahadhari pekee watu watazingatia ni betri low katika simu zao 🙃

25. Karibu bongo ambapo Nyumba iliyo andikwa tunauza ice cream hapo kabla paliandikwa "OGOPA KUNA MBWA MKALI", kwa sasa mabinti zao wapo nyumbani na hakuna mwanaume ambaye anaenda kupeleka posa.🤗

26. Karibu bongo ambapo watakusimanga ukiwa hai ila ukifa watasema ulikuwa mtu wa watu na kuja na kauli kuwa marehemu hasemwi vibaya🤐

27. Karibu bongo ambapo watu watapika pilau na kununua jeneza zuri ili wakuze wakati ulikufa kwa kukosa pesa za matibabu 🙁

28. Karibu bongo ambapo wasomi wanatumia vyeti kupata kazi na maarifa yakiwa kwa watu wasio wasomi.😕

29. Karibu bongo MTU ana followers 20k kwenye social media lakini hakuna anayempa mchongo wa kazi au shughuli ya kipato😌

30. Karibu bongo ambapo kuna katika ukoo mwenye maisha mazuri ndio mtunza hazina wa ukoo😮
 
Kuna wakati nikiwa Dar nilikuwa napita sana maeneo ya soko la wamachinga Karume. Pale pembeni kuna kijiwe kimoja maarufu sana cha kahawa na watu makumi kwa makumi ujazana pale kujadili mpira hasa timu za Yanga na Simba kutwa nzima. Yaani pale hadi watumishi mashabiki wa mpira uchomoka kutoka maofisini kwenda kusikiliza uchambuzi wa mpira unaofanywa na wabobezi huku mjadala ukisimamiwa na viongozi kabisa. Uwa najiuliza kijiwe hicho na vingine vya aina hiyo kama vipo kama wangekuwa wanajadili hatima ya nchi kisiasa na kiuchumi kama vile vijiwe vya majirani zetu Kenya si tungekuwa tumeshapata uelewa mpana kama Gen Z na kupata katiba mpya na pia kuifanya serikali kulinda maslahi ya taifa tofauti na hali ilivyo sasa.
 
Kifupi bongo ukiwa na akili nyingi ni hasara. Chamsingi hii nchi omba uzima, akili kama za Mwijaku zinatosha sanaa, kutoboa nje nje
 
Dah! Umepiga mule mule baadhi ya namba zimenitaja Mimi 😔
 
Back
Top Bottom