Hii ni zaidi ya kichwa cha mwendawazimu: Everton Yaichabanga ATV Irdning kwa magoli 22 - 0

DonDonald

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,533
Reaction score
2,709
Timu ya soka ya Everton ya Uingereza yaifunga timu ya ATV Irdning ya Austria kwa mabao 22 - 0 ndio mabao ishirini na mbili kwa bila.

Katika mechi hiyo ya kirafiki wachezaji wanne wa Everton walifunga Hat -Tricks, Mirallas aliyefunga magoli 5, Tosun aliyefunga magoli 4, Niasse aliyefunga magoli 4 na Lookman aliyefunga magoli 3.

Katika dakika 17 za mwanzo wa mchezo Everton walikwisha funga magoli 6, mpaka mapumziko walikuwa wanaongoza kwa magoli 10 kabla ya kufunga magoli mengine 12 kipindi cha pili.

Mirallas aliingia kipindi cha pili na akafunga magoli matano peke yake

Pia katika mechi hiyo Everton walifunga magoli mengine 3 yaliyokataliwa na mwamuzi wa mchezo huo.

 
ATV ipo daraja la ngapi mkuu? Kuna sehemu nmeona ipo 5th level ya Austria football,, So sio kitu cha maajabu sana ukilingansha na Everton yenye historia kubwa kwenye soka la England
 
ATV ipo daraja la ngapi mkuu? Kuna sehemu nmeona ipo 5th level ya Austria football,, So sio kitu cha maajabu sana ukilingansha na Everton yenye historia kubwa kwenye soka la England

Sina uhakika hiyo timu ipo daraja la ngapi, ila lazima itakuwa ni kutoka madaraja ya chini.

Usisahau kuwa hizi timu "Kubwa" kila kabla ya msimu kuanza zinachezaga na timu hizi "Ndogo", ila ni nadra kuona matokeo kama haya.

Arsenal jana kacheza na timu ya Boreham Wood inayoshiriki ligi ya daraja la 5, matokeo Arsenal alishinda 8 - 0, kwahiyo kwa walichokifanya Everton ni kitu kikubwa kwao {Ni Rekodi yao ya kushinda magoli mengi katika mechi moja}
 
Najiuliza hyo Tim ilikua na golkipa
Kweli maana co Kwa kulala huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…