vijana tuliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, tumekuwa kama specimen kwa ajili ya majaribio ya wizara ya elimu, hili swala la kutotolewa selections mpaka sasa hivi, linatuumiza sana hasa kwa wale tusio na uwezo wa kumudu gharama za shule binafsi, ningeomba hawa watu wa wizara wajaribu kuangalia athari zilizopo huku mtaani hasa kwa mtu asiye na kazi yoyote ile, ni mwezi wa 9 sasa toka tumalize shule.
Pia hawa watu wanaojihita wadau wa elimu wasisubiri matokeo mabaya, ndio walalamike, wajaribu kuangalia na hili swala.