informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Uwepo wa Ukumbi wa muziki ambap pia una baa ndani yake (Night Club & Bar) uliopo kwenye eneo la Hifadhi ya Mto Kanoni ni jambo ambalo inaonekana kama mamlaka husika zinazotoa vibali vya ujenzi limefumbia macho wakati uhalisia eneo hilo linaonekana sio salama kwa Watu.
Awali katika eneo hilo kulijengwa baa lakini baada ya muda ikazuiwa kutokana na kubainika ujenzi ulivuka mipaka kwa kuingilia eneo la hifadhi ya Mto huo.
Katika mazingira hayo ambayo yanaibua maswali juu ya uwajibikaji wa mamlaka husika zinazotoa vibali, imekuwaje tena eneo hilo ikajengwa club ambapo miundombinu ya kuta imefika kabisa kwenye kingo za Mto!
Hata hivyo ujenzi huo umefanyika ikiwa kuna kibao kinachoonesha na kutoa marufuku na tahadhari kwa Mtu yeyote kutofanya shughuli zozote za kibinadamu eneo hilo.
Sasa najiuliza, mhusika ambaye ameratibu ujenzi huo yupo juu ya Sheria? Kwanini anakingiwa kifua au mbuyu umezungukwa?
Wito wangu kwa mamlaka husika zinazotoa vibali ikiwemo NEMC lakini pia TAKUKURU wafuatilie suala hilo na kuchukua hatua za haraka.
Ikizingatiwa kwa mara kadhaa katika eneo hilo la Mto Kanoni kumekuwa kukitokea mafuriko ambayo yanasababisha athari mbalimbali kwa wananchi walioko maeneo ya karibu.
Kwani pamoja na jengo hilo kuwa hapo, ikumbukwe kuwa kumekuwepo na mpango wa uboreshaji wa kingo za Mto Kanoni kupitia Miradi ya Kupendezesha Miji (TACTIC) Manispaa ya Bukoba, hivyo uwepo wa sehemu hiyo ya starehe inawezekana ikawa kikwazo kwa mradi.
Inadaiwa jengo hilo linamilikiwa na Mwenyekiti wa CCM Bukoba Mjini, Muganyizi Zachwa kama ni hivyo kweli basi yeye anatakiwa kutafakari na kufikiria usalama wa watu wengi wanaofika eneo hilo kwa ajili ya kuburudika.