Hii nyimbo

Hii nyimbo

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
huwa nakereka mpaka basi. Wanasema waungwana, uongo ukirudiwa sana huwa ukweli. Mbaya zaidi upotoshaji huu huanzia studio na vituo vya redio na tv. Msanii anasema 'hii nyimbo yangu nimeirekodia mj. Nina nyimbo zingine 3 ziko jikoni...' Shule gani hawa bazazi wamesoma? Hawawezi kutofautisha wingi na umoja?

Mwingine utamsikia 'huu mwimbo'. Ugumu uko wapi kutamka 'huu wimbo' na 'hizi nyimbo?' Kuna upotoshaji mwingi pia ila kwa leo nimeona hili
 
"Iliyopo hewani ni nyimbo mpya wa Mwana FA ficharingi FidQ ......"
 
kusema ukweli mi pia nakereka sana

kama kuna uongo ambao umerudiwa sana tena kwa MAKUSUDI (maana siamini kama huwa hawajui kuwa neno msahihi ni wimbo na sio nyimbo wakimaanisha umoja) ni huu. sasa sitaki kuamini kuwa BAKITA na TUKI wamekubaliana na hili!

badala ya kuhangaika na 'hakunaga' wangefungia kwanza wale wote wanaopotosha hili neno. Huwezi kusema 'hii nyimbo yangu nimeiandika mwaka jana" badala ya "huu wimbo wangu" na labda "albamu yangu itakuwa na nyimbo kumi"
 
ndo hivyo tena. Upotoshaji umerudiwa hadi umekubalika. Sijawahi kusikia popote hawa wenye mamlaka wakikemea hili.
 
Ndo kiswahili kinakuwa, upotoshaji, utohoaji. Wenyewe si wanaziitaga rejesta za mitaani sijui!
Kazi kwenu, ndo kibongo fleva bongo fleva hicho
 
Dah!Kweli lugha yetu hadhimu hadhi yake inaporomoshwa na wa2 wachache...Cjui TUKI,TAKILUKI,BAKITA,BASATA n.k. wana fanya nini katika ofisi zao au wananepesha ma2mbo yao....Wangetoa walau mchango wa elimu ya sarufi ya lugha kwa wasanii wetu, hii ingeweza kusaidia.
 
Mkuu afadhali umenena, BAKITA aka Baraza la Kiswahili Tanzania is a toothless bulldog, wanaacha kiswahili kinachezewa Kama mwasesere. Redio ndio zinazoongoza kwa kuboronga utasikia kipindi kimesababishwa na airtel badala ya kusema kimedhaminiwa, utasikia majiji badala ya miji. Kuwe na ulazima kuwa , kufanya kazi media lazima Mtu awe na ufaulu wa lugha adimu ya kiswahili.
 
"Iliyopo hewani ni nyimbo mpya wa Mwana FA ficharingi FidQ ......"

Hapo wanasema fiucharingi,kuna msanii anaitwa Barnaba anavunja kingeleza kinoma

1.Kuna siku ashawahi sema yeye ni celebrate(I'm celebrate)

2.Kuna kipindi alikua marekani akahojiwa live akachemka tena kwamba wanafanya training ili waje kua good leadership

3.Juzi Juzi aliulizwa na Kayanda,vp hali yako mr barnaba? Naye akajibu kwa kingeleza "ohh I was good" kayanda ikabidi ayeyushe kwamba Naona siku hizi unajua kuongea kiswahili vizuri

NB:meneja wake amshauri dogo asiwe anaongea maneno ya kingeleza bila kujua,au kama anakipenda aende British Council akale nondo
 
Dah!Kweli lugha yetu hadhimu hadhi yake inaporomoshwa na wa2 wachache...Cjui TUKI,TAKILUKI,BAKITA,BASATA n.k. wana fanya nini katika ofisi zao au wananepesha ma2mbo yao....Wangetoa walau mchango wa elimu ya sarufi ya lugha kwa wasanii wetu, hii ingeweza kusaidia.
na wewe pia jaribu kunyoosha hii lugha adhimu
 
Hapo wanasema fiucharingi,kuna msanii anaitwa Barnaba anavunja kingeleza kinoma

1.Kuna siku ashawahi sema yeye ni celebrate(I'm celebrate)

2.Kuna kipindi alikua marekani akahojiwa live akachemka tena kwamba wanafanya training ili waje kua good leadership

3.Juzi Juzi aliulizwa na Kayanda,vp hali yako mr barnaba? Naye akajibu kwa kingeleza "ohh I was good" kayanda ikabidi ayeyushe kwamba Naona siku hizi unajua kuongea kiswahili vizuri

NB:meneja wake amshauri dogo asiwe anaongea maneno ya kingeleza bila kujua,au kama anakipenda aende British Council akale nondo
kingeleza sio
 
kwetu sisi nyimbo na wimbo sawa sawa tu. Sema hilo neno wimbo ni km la zamani zaidi.
 
Znz, Unguja mjini

kwanza unguja hakuna hilo jina, japo la bandia. Pili japo kiswahili fasaha kimetoka unguja, isiwe sababu ya kutupotoshea kiswahili sie wa barai. Nyimbo ni wingi. Wimbo ni umoja
 
Ni kweli, jina langu asili yake ni kwengine lkn nimekulia Unguja na kusoma huku.
Kuh neno wimbo sawa mkuu nimeelewa ndo twajifunza hivo kwani maisha ni kusoma
 
ni vizuri kuwa umeelewa. Kawafundishe na waunguja wengine pia
 
Back
Top Bottom