Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
we unaona sawa?"Iliyopo hewani ni nyimbo mpya wa Mwana FA ficharingi FidQ ......"
huwa nakereka mpaka basi. Wanasema waungwana, uongo ukirudiwa sana huwa ukweli. Mbaya zaidi upotoshaji huu huanzia studio na vituo vya redio na tv. Msanii anasema 'hii nyimbo yangu nimeirekodia mj. Nina nyimbo zingine 3 ziko jikoni...' Shule gani hawa bazazi wamesoma? Hawawezi kutofautisha wingi na umoja?
Mwingine utamsikia 'huu mwimbo'. Ugumu uko wapi kutamka 'huu wimbo' na 'hizi nyimbo?' Kuna upotoshaji mwingi pia ila kwa leo nimeona hili
kusema ukweli mi pia nakereka sana
kama kuna uongo ambao umerudiwa sana tena kwa MAKUSUDI (maana siamini kama huwa hawajui kuwa neno msahihi ni wimbo na sio nyimbo wakimaanisha umoja) ni huu. sasa sitaki kuamini kuwa BAKITA na TUKI wamekubaliana na hili!
badala ya kuhangaika na 'hakunaga' wangefungia kwanza wale wote wanaopotosha hili neno. Huwezi kusema 'hii nyimbo yangu nimeiandika mwaka jana" badala ya "huu wimbo wangu" na labda "albamu yangu itakuwa na nyimbo kumi"
"Iliyopo hewani ni nyimbo mpya wa Mwana FA ficharingi FidQ ......"
na wewe pia jaribu kunyoosha hii lugha adhimuDah!Kweli lugha yetu hadhimu hadhi yake inaporomoshwa na wa2 wachache...Cjui TUKI,TAKILUKI,BAKITA,BASATA n.k. wana fanya nini katika ofisi zao au wananepesha ma2mbo yao....Wangetoa walau mchango wa elimu ya sarufi ya lugha kwa wasanii wetu, hii ingeweza kusaidia.
kingeleza sioHapo wanasema fiucharingi,kuna msanii anaitwa Barnaba anavunja kingeleza kinoma
1.Kuna siku ashawahi sema yeye ni celebrate(I'm celebrate)
2.Kuna kipindi alikua marekani akahojiwa live akachemka tena kwamba wanafanya training ili waje kua good leadership
3.Juzi Juzi aliulizwa na Kayanda,vp hali yako mr barnaba? Naye akajibu kwa kingeleza "ohh I was good" kayanda ikabidi ayeyushe kwamba Naona siku hizi unajua kuongea kiswahili vizuri
NB:meneja wake amshauri dogo asiwe anaongea maneno ya kingeleza bila kujua,au kama anakipenda aende British Council akale nondo
kwetu sisi nyimbo na wimbo sawa sawa tu. Sema hilo neno wimbo ni km la zamani zaidi.
Znz, Unguja mjinikwenu sayari gani? Msituharibie lugha tafadhali
Znz, Unguja mjini
Ni kweli, jina langu asili yake ni kwengine lkn nimekulia Unguja na kusoma huku.kwanza unguja hakuna hilo jina, japo la bandia. Pili japo kiswahili fasaha kimetoka unguja, isiwe sababu ya kutupotoshea kiswahili sie wa barai. Nyimbo ni wingi. Wimbo ni umoja
Ni kweli, jina langu asili yake ni kwengine lkn nimekulia Unguja na kusoma huku.
Kuh neno wimbo sawa mkuu nimeelewa ndo twajifunza hivo kwani maisha ni kusoma