Nduka Original,
Uzi wako naufuatilia tangu asubuhi. Kwanza nakupongeza kwa kuwa muwazi sana. Hauko peke yako kwani kuna wenzio humu wengi tu kazi hizi zimewashinda lakini wanabadili kila siku. Pongezi kwa kueleza ukweli wako.
Watu wana hasira na wewe kwa sababu unajipa mateso yasiyo na sababu. Acha kwamba si jambo zuri kidini lakini pia kijamii. Hayo nakuachia mwenyewe. Ila wajua wanakasirika nini? Kama Mkuu Mbu na wengine walivyosema hapo juu,uwezo wako haukuruhusu kufanya ufanyayo. Sitaki kurudia kuwa aidha umeshapata usaidizi nyumba kubwa (na anakudanganya anaridhika) na nyumba ndogo utapata karibuni. Usipoangalia, wanao ni yatima watarajiwa!
Siku moja nimeongea na jamaa yangu ana duka la dawa. Alinielezea jinsi amabavyo wanaume wa kuanzia km 40 and above wanavyokuja kununua dawa zinazoweza kuwasaidia "kuwawezesha". Anagalia matangazo magazetini na barabarani yahusuyo nguvu za kiume. Wamasai wanauza dawa,haiyumkini ni unga tu au randa za mbao lakini hewala watu wanajitosa walau ziwasaidie.
Tatizo ni kubwa na ilishasemwa hapa ktk uzi fulani. Tupunguze kula vibaya,mavitambi na mazoezi ni lazima. Si lazima gym hata ruka kamba basi. Mtu biaaa na chips mayai mwanzo mwisho halafu unategemea nini?
Sikupi pole, sikuhurumii. Shauri yako. Umejitega na unaweza kujinasua. Umejitia aibu na trust me,keshawaambia rafiki zake na serengeti boyz hauwezi kitu. Hata mkeo unayemmegea anakusema. Hapa unajificha ila mtaa mzima wanajua hauwezi kitu.