Hii Restaurant ni yaje, ni yaje Aiseeeh

Huu msemo wa kipumbavu muasisi ni nani? Mbona naona mpaka watu wa heshima wanajivua nguo katika hili?

Muasisi ni MPENJA,,, yule wa Azam...

Amekuwa akisema hvo kipindi timu ikishida,,, huchombeza kwa kusema.. "kwani timu pinzani Yanga yenyewe insemaje"...

Sasa watu wameufanya ukue na kuutumia hata pasipotakiwa...

Tukae humo...kama hujaewa, Nyoosha mkono uliza
 
Huu msemo wa kipumbavu muasisi ni nani? Mbona naona mpaka watu wa heshima wanajivua nguo katika hili?
Ha ha ha Dah ! Mkuu kumbe nawe unauchukia km unavyonikera mm
Yaan unaniudhi huu msemo dah !
Yaan kwakweli misemo ya kijingajinga dizaini hii huwa inaniudhi sana
Maana jana tulikuwa tunajadili jambo group ya WhatsApp basi bana kuna mtu tena mtu mzima tu na familia yake ndo akaingizia huo msemo
Bwana watu walimshukia kumbe ni wengi tusiopenda misemo ya hovyo namna hii
 
Ni mambo ya kitoto sana ambayo watu wazima kuendekeza au kujihusisha nayo ni upuuzi na kujivua nguo!
 
Huu msemo wa kipumbavu muasisi ni nani? Mbona naona mpaka watu wa heshima wanajivua nguo katika hili?
Mimi kuna huu na ule " kimeumana" yaan mpaka nasikia kutapika hata kama ni mdada unaongea hivi sembuse mwanaume[emoji57][emoji57]

Wanaume rijali vitu vingine vinavyoletwa n juma lokole mviache huko instagram mweeh aibuu
 
Aibu kweli kweli yani imekuwa kama slogan! Left & Right “Kwani.....inasemaje?” Ushoga huu!
Huo kimeumana nilikuwa nausikia ila not so often kama huu wa kipumbavu. Hata Mc Garabat anutumiaga
 
Ni misemo tu tena itapita km ilivyopita misemo mingine na kwasasa hata haitajwi sion km kuna haja ya kuumizwa na hii misemo
 
Huu msemo wa kipumbavu muasisi ni nani? Mbona naona mpaka watu wa heshima wanajivua nguo katika hili?
Ila mkuu mbona hujaonyesha Imoji ya kukasirika yani ww huwa ni kucheka tena sio kucheka tuu kucheka kujigaragaza hahahahaaaha
 
Kuna pia hili neno "kipengele" Ila nashukuru Sasa hivi limepotea. Liliwahi kunifanya nikamkatia mtu mawasiliano mazima
Afadhari kipengele huo kidogo hupenda kutumia madalali hasa madalali wa magari
Wana msemo wao mmoja
Dah ! Eti narenga narengesha hiyo IST haina kipengele inatakiwa 7 tuishi humohumo

Ha ha ha
 
Huu msemo wa kipumbavu muasisi ni nani? Mbona naona mpaka watu wa heshima wanajivua nguo katika hili?
Nimeshangaa hadi huyu dingi amevua Shati, suruali,naona anataka kutoa na boxer yake sijui ili iweje
 
Afadhari kipengele huo kidogo hupenda kutumia madalali hasa madalali wa magari
Wana msemo wao mmoja
Dah ! Eti narenga narengesha hiyo IST haina kipengele inatakiwa 7 tuishi humohumo

Ha ha ha
Huo wa kipengele hata mie nautumiaga sometimes sioni shida yake kimantiki! Ni neno ambalo lina maana sawa na ugumu, au obstacles! Sio neno la kishambenga bali ni neno practical kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…