Hii sarafu ya tshs 500 inaashiria kukua au kuanguka kwa Uchumi?.

lengume

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
318
Reaction score
134
Mimi sio mtaalam wa mambo ya Kiuchumi lkn kwa uelewa wangu naamini Nchi kuendelea kutengeneza fedha kubwa huko kunaonyesha Uchumi kuharibika.

Kwa mfano Nchi ya Kenya fedha zake ziko juu sana ukilinganisha na Tanzania. eg Kshs 100 ni sawa na tshs 1870. Utaona ni kwa jinsi gani tulivyozidiwa.

Upande wa Kenya noti kubwa kabisa ni ya shs 1000 wakati ya Tanzania ni shs 10,000. kwa upande wa Sarafu shs 40 ndio Sarafu kubwa kabisa Kenya wakati Tanzania ni shs 500.

Mimi ninachojiuliza, hawa Watu wanaojiita Wachumi hapa Tanzania huwa kazi yao kubwa ni nini wakati Uchumi unaendelea kudorora?.

Naomba kama kuna mtaalam au wataalam wa Uchumi watuambie nini maana ya kuendelea kutengeneza sarafu kubwa badala ya kupunguza ukubwa wa Fedha?. Nategemea sana mchango wenu.
 
Ni kwamba wanauchumi wapo,na ushauri wao hauwapendezi wanasiasa. Wanasiasa ndio waamuzi wakuu hata kama ni jambo la kuathiri uchumi au uhai wa nchi.
 
ngoja wataalam waje watu chambulie mada hii....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…