SoC04 Hii sio ya kufikirika tena kwa hulka bali kuona

SoC04 Hii sio ya kufikirika tena kwa hulka bali kuona

Tanzania Tuitakayo competition threads

Auntyg

New Member
Joined
Jun 8, 2023
Posts
3
Reaction score
4
Si hayo unayofikiri kuwa, bali ni mambo yaliokuwa ni hulka Kwa waja na kuwa ahadi yenye thamani kama Vito, iliyoaminika kuwa ni ndoto ya abunwasi kumbe hata Malkia mchwa anaweza kufanya ikiwa yeye ndio mfalme na sauti ya kuwatiisha waja

Ni viumbe wenye ushirika mkubwa sanaa ila balaa lao sio dogo . Hufanya kazi Kwa amri ya Malkia Kwa umoja kutoka mwanzo Hadi tamati na Kwa upendo, lugha Yao ni moja huelewana wao Kwa wao tu katika ardhi Yao .isiyo na tafrani hata mara Moja.

Malkia mchwa hupenda maendeleo ya wafuasi wake na hawapendi ugomvi , sikuzote wapo kwenye msafara wa kutafuta na kuenenda kwenye ujenzi wa ardhi yenye maziwa na asali Kwa utulivu .ambayo ni matamanio yao

Ikiwa Malkia yeye ndio msemaji Kwa wafuasi wake ,alitamani sana nchi yake iwe ni nchi ya maziwa na asali. Lakini kutokana na maumbile madogo ya wafuasi wake , na idadi ya kuzaliana ni kubwa lakini alijipa moyo Kwa hakuna jambo la kushindikana haijalishi ,maumbile tuliyo nayo na mchwa wenzangu , na mawazo finyu lakini Mimi kama Malkia natoa tamko rasmi

Ili badae tuishi kwenye ardhi ya maziwa na asali yenye kuvutia machoni pa waja, bila kujali udogo wa maumbile na uwezo wetu kama timu yote ya wafuasi wote .Tufike nchi ya ahadi kama ifuatavyo

@ Wadudu Hawa walijihami Kwa umoja na kuwekeza nguvu katika ujenzi wa vichuguu vingi na imara .
Tamko la Malkia ni kupata Makazi , na vichuguu huwa na ramani ya nzuri zenye kiini macho Kwa waja na yenye kuvutia waja kutoka sehemu mbali mbali za misitu ,hivo mchwa hugawana majukumu kama Injinia / kandarasi hivo kutokana na uwezo mdogo waliokuwanao ilichukua miaka kadhaa (pole pole ndio mwendo )na katika ujenzi wa vichuguu virefu na imara , pia Kwa ajiri ya wageni kivutio kwao,na miradi mingine na muonekano mzuri wa mandhari

672df53bb8852a222babf57f92ba14d5(0).jpg

Picha: kutoka Tanzania safari channel

Pichani
: ni kichuguu kikubwa na imara kilichojengwa na mchwa , ukilinganisha na umbile ya mchwa imegharimu miaka mingi lakini. Mjengo mithili ya ghorofa lenye ramani nzuri za kiini macho .

Malkia mchwa tamko lake ni amri katika utawala wake ulio thabiti
Vichuguu hivo vitasaidia sana kupata Makazi ya muda Kwa watalii , pia Makazi kama hospital katika kila eneo la nchi hio iliyotawaliwa na mchwa ,baadhi ya vichuguu vilikuwa na miradi mbali mbali Ili wafikiie Yale matamio ya nchi yenye maziwa na asali na yenye mandhari nzuri hata katika msafara yetu ,sisi mchwa kurahisisha njia mbali mbali zisaidie pindi tunaenda kutafuta chakula

B)Kupitia kiti cha Malkia mchwa aliitisha vikao mara Kwa mara na wafuasi wake kadhaa... Kuwekeza kwenye miradi Hasa ya mazao . Isiyogharimu mtaji wa kulipa . Malkia mchwa hujua kwamba wao wamebarikiwa udongo wenye rutuba hivo yatupasa kuwekeza kwenye mazao/kilimo Kwa kasi sanaa maana ndio ukwasi tulionao

Kutokana na utawala thabiti wa Malkia mchwa. Wafuasi wake pia walitamani wafike ardhi Ile ya ahadi. Tupo safarini Wafuasi wengi walijishughulisha na kilimo na mazao mengi walipata ya kula na malighafi Kwa wingi . Na faida yingi zilienda kwenye maandalizi ya madhari ya ardhi Ile

C) Malkia mchwa aliandaa sera zinazo himiza maboresho ya mandhari / miundombinu inayo tuzunguka bila kujali udogo wa mchwa na mapato Bado ni madogo( kuthubutu)

"Tunathubutu , tunafanya na daima tutasongambele"
Malkia mchwa alitumia ujasiri mkubwa Kwa maono aliyonayo
Wafuasi watakiwa kile kidogo kinachoingizwa katika mapato ya nchi taratibu ujenzi unaendelea tupate njia nyingi Kwa mchwa Wanazaliana Kwa wingi na idadi inazidi kuwa kubwa. Mchwa hujitahidi kuendana na sera ya Malkia mchwa ili ifikapi tamati waishi kwenye ardhi waliiyokuwa wa kiifikiri Kwa matamanio na iwe yenye kutazamwa asilia
Kwa umoja wa mchwa huwa na msafara wa kusaka chakula, udongo mzuri wa ujenzi, Ili kutimiza haja walio nayo "umoja ni nguvu ". Mchwa hujenga Kwa kutumia mate, kinyesi na punje za udongo
3c-670x430.jpg

Picha:kutoka chakupewa tv

Pichani ni mchwa katika ushirika Kwa ktengeneza miundombinu ,ambayo huchukua takribana miaka zaidi ya 5 kutoka na kasi ndogo na nguvu ndogo na hutegemeana hivo hukamilisha hitaji lao Kwa miaka kadhaa

Malkia mchwa anatakiwa kutumia kiti chake katika mipango ya maendeleo Kwa utawala thabiti anafanya wafuasi wafike Ile nchi waliokuwa walitamani kuwa yenye mandhari inayovutia . Japo mchwa wanauchumi mdogo ila Pole pole ndio mwendo hivo , Malika mchwa. Huandaa Ramani za njia mbali mbali ndani ya kichuguu kurahisisha. Kujongea .na kupunguza foreni

Pamoja udogo wa uchumi wao Malkia mchwa huwa na kamati yake ya ushauri yenye nguvu na amri kisheria.

Utawala thabiti ndio chanzo Cha maendeleo yetu na ardhi yetu iwe nzuri ya kuvutia
Termite-mound-1.jpeg

Picha:kutoka Tanzania safari channel

Barabara zimejengwa japo Kwa muda mrefu sanaa lakini ni imara mithili ya fryover. Hivo imerahisisha .misafara ya mchwa katika shughuli mbali mbali za waja
Wahenga husema.
"Hayawi hayawi Sasa yamekuwa"
Ile ardhi ya maziwa na asali ndio hii Sasa. Tumeweza na tutazidi kusongambele
Mandhari inavutia mchwa wote

Mjue kiongozi Malkia mchwa mwenye tamko lake inawezekana
Fsm2p-IWIAkA80Y.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom