Hii stand kuu ya Arusha ni aibu kwa Rais wa nchi

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Mji wenye pilika nyingi km Arusha unakuwaje na kastand kadogo kazamani km hii iliyopo? Utaambiwa kuna ubishani kati ya mbunge na viongozi wengine wa mkoa.

Wananchi ndio wenye nchi ndio wanaotumia stand nchi ina Rais eti pesa ipo na eneo lipo kule bondeni city ujenzi hauanzi, we Rais unajionaje?

Ndio maana watu wanashindwa kumsahau Magu, tunajua Gambo ana arrogance lakini ni nyau tu. Magu angetoa agizo tu na muda wa kuikamilisha wangefanya kazi usiku na mchana, vinginevyo warudi kwao.

Mji wa Mwanza stand kubwa 3; Buzuruga, Buhongwa na Nyegezi, Arusha kuna siasa za kishamba sana. Rais wasaidie wananchi wako stand kuu kubwa ya kisasa ijengwe.

Wasiwasi wangu wale wafanyabiashara wakubwa wa mjini kati wana mikono yao wanatumia viongozi km kina Gambo, ni akili finyu sana kukwamisha maendeleo ya nchi kwa maslahi ya watu wachache.
 
Gambo anazuiaje ujenzi wa stendi hapo Arusha mkuu
Maokoto... Stendi ya awali ilikuwa ijengwe Olasiti mwisho...wakabaini ilikuwa ni plans za Gambo na genge lake kupiga pesa.
Wajanja pale Manispaa nao wakampata Mhindi wao kule maeneo ya Oljoro JKT wakapeleka proposal stendi ihamie kule. Proposal ikapita kwa sharti kwamba Mhindi awape viwanja kadhaa vya bure kwa matumizi yao binafsi ili vinavyobaki ndo vitumike kwenye ujenzi wa stendi.

Gambo na genge lake wakahisi kuzidiwa maarifa!
Ndo hivyo sasa. Stendi Mpya itajengwa almost 15KM kutoka ilipo ya sasa.
Swali linakuja sasa: Je, kwa miondombinu na mitandao ya barabara zinazounganisha Arusha na mikoa mingine STENDI MOJA TU INATOSHA?

Kwa wageni wa mjini wa Arusha... stendi mpya inataka kujengwa uelekeo tofauti kabisa na barabara kuu zilizopo (Arusha-Nairobi, Arusha-Babati-Mwanza, Arusha-Moshi-Tanga-Dar).
Bila ubunifu taabu itabaki mle mle!
 
Mbeya wanahela and sio wabahili,Arusha/Moshi km sio ukoo wao hata Maji yakunywa unaweza usipewe,Makonda anakazi sn kule juu
 
Shida ya stand ya Arusha wanafanya parking hapo.

Trafik wapo hawafanyi lolote, kuna siku ikabidi nipate maoni ya wadau ikaonekana ni rushwa tu zinatembea tu.

Kwa lile eneo kama kunakuwa na matumizi mazuri kwa maana ya stand linaweza lisilete changamoto sana.
 
Heee umeuona?? Uliiona wapi, hakunaga
 
Uelekeo tofauti kabisa na miundombinu hakuna
 
Ila ikijengwa utasikia mama ametufikia, mama ametujengea, mama amewekeza, mama blah blah...
 
Huo ndiyo ukweli kunatakiwa lipite panga la kusafisha kwa kuhamisha watendaji wengi hasa wa ardhi.
 
Ile proposal ya kujengwa eneo la SADC kwenye mashamba katikati ya tengeru na USARIVEr iliishia wap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…