Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
kulikukuwa na watu wawili mtu na mke wake. watu hao walikuwa masikini wa kutupwa. siku moja walitembelewa na mtu aliyekuwa akisafiri. walimkaribisha kwa ukarimu na akalala hapo. mgeni huyo aliguswa sana na umasikini wa watu hao. asubuhi wakati anaondoka aliwaachia pete. aliwaambia wanaweza kuiomba mambo yoyote matatu na watapata. Kisha akaaga na kuendelea na safari.
mke wake akamwambia mumewe "mi naenda kuchota maji nikirudi tutajadiliana cha kuomba''. mkewe alivyoondoka jamaa huku alikuwa akiishika shika pete kisha akasema "pete naomba pilau kuku". Saa ileile pilau kuku ikatokea na jamaa akaanza kujichana. mke alivyorudi akashangaa na kuuliza "mme wangu umepata wapi pilau". jamaa akajibu ''nimeiomba pete". kusikia hivyo mke wake alipandwa na ghadhabu na kusema "badala ya kuomba vitu vya maana unaomba pilau! litakupeleka wapi" kisha kwa hasira kali akasema "pete naomba mume wangu awe na kichwa kama cha jogoo". Muda ulele jamaa akawa na kichwa kama cha jogoo na mwili wa mtu.
baada ya muda kupita yule mama hasira zilimuisha na akaanza kumuonea huruma bwana wake. mwishowe akasema ''pete naomba mume wangu arudi kama zamani". Basi yule mume alirudi kama zamani na ile pete ikapotea.