Hii verse ya tatu ya Joh nimeilewa sana

bizzle11

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
246
Reaction score
198
Sipenzi mawazo Ya kupewapewa
Na ndo mana mi sipendi bure
Sipendi ukoloni hasa mkoloni mweusi
Na ndomana joh mi siendi kule
Ili tu mi nile zile chuki zile
Hunijui kivileNyani haoni kundule
You kiss ass na mnabaki na dhiki deile
Na misa za kanisa mko siti za mbele
Ni msasa nakuna kama kuna vipele
Nami sa-sinafichua kama deutsche-welle Wanasiasa hawamwachii mungu wanajipa madaraka
Nyumba za ibada hazimwachi kukusanya sadaka
Nami simwachi kujitoa uswahilini kwenye taka
Niko vitani kipande cha keki yangu nataka Am on my own lane Am on my own plane
 
Kwenye airport moja huko Japan wameweka kioo kikuubwa, ukisimama mbele yake kinataja jina lako na nchi unayoelea.

Mpemba mmoja akasimama mbele ya kioo akaambiwa jina lake ni Awadh Mkufu Mbaruku na ndege yake inaelekea Zanzibar.

Mpemba alishangaa sana, akaona ngoja ahakikishe kama kioo hakikubahatisha. Akavua koti akavaa kanzu, kilemba na miwani. Akarudi tena mbele ya kioo akaambiwa jina lake ni Awadh Mkufu Mbaruku na ndege inaelekea Zanzibar.

Mpemba akaenda kuvua kanzu akavaa zawadi alizomnunulia mkewe. Akavaa night dress,akapaka rangi za midomo, akatafuna kungu na kulegeza mwili. Akarudi tena mbele ya kioo, akaambiwa,"Jina lako Awadh Mkufu Mbaruku na ndege yako ishakuacha kwa ukhanithi wako".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…