Hii video ndiyo iliyomfanya Askofu Kakobe anyang'anywe passport?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Jamaa ameumizwa sana kwasababu tu alitaja Tanganyika. Imagine, tangu enzi Wazanzibar wapo huru kujivunia Zanzibar na kupigania Zanzibar, wana serikali yao, bunge lao, lakini mtu wa Bara akitaja Tanganyika anachokutana nacho ni hatari tupu.

Hutakiwi kujiita mtanganyika, ila wengine wajiite tu wazanzibar. nyerere aliweka uoga wa ajabu sana na bado watu wanaishi kwenye kivuli hicho.

Imefika muda sasa kilichopo mioyoni mwa watanganyika kijadiliwe kwa uwazi na muafaka ufikiwe.

siku zote yupo hapo mwenge. wala hakwenda nje. ila kati ya watu walionyanyaswa sana na serikali hii, huyu mmojawapo. wanaojua wanajua. ajabu alikuwa anaongea maneno haya ndio yaliyomponza, alichosema alisema it is just a matter of time, na ile time ndio imefika sasa.
 
ALITABIRI KUWA ITAFIKA WAKATI MUUNGANO UTAKUWA DHAIFU NA WATANGANYIKA WATAITAKA NCHI YAO

SEREKALI IKAMBEZA NA KUMTISHIA KUMBE IT WAS A TICKING BOMB

THE TIME IS NOW, ITS TOO LATE
 
Mijadala ifanyike bila ya hofu ifanyike kila mahali

Serikali tatu au Serikali ya mkataba nk.

CCM imekuwa ikituaminisha kuwa ni taboo kujadili Muungano tuutakao hizi sio zama za giza.
 
Ukiwa Mtanganyika unakuwa ni raia wa Uingereza Automatic, wengine Utanganyika wetu ulitusaidia sana.

Sasa Muingreza kawachoka, mtamlaumu bure Nyerere, mchawi wenu ni Muingereza.
 
SASA wewe mla urojo wa zenji, Tanganyika inakuhusu nini sasa? nyamaza watu wawafanye wilaya ama la sote tufutike ibaki Tanzania.
 
Mijadala ifanyike bila ya hofu ifanyike kila mahali

Serikali tatu au Serikali ya mkataba nk.

CCM imekuwa ikituaminisha kuwa ni taboo kujadili Muungano tuutakao hizi sio zama za giza.
watu waachwe wajadili kwa uhuru, mambo ya kutiana hofu kama kipindi cha nyerere ndio huleta majipu yakipasuka inakuwa kama libya. mtu kama kiongozi zuia siku zote kuminya uhuru wa kuongea, watu wasipoongea utajuaje kilichopo mioyoni mwao? kwanza wanakuwa wanakusaidia kujua nini yakupasa kufanya.
 
Mfumo wa Serikali tatu hauna ubaya wowote.
 
ajekuanzisha kanisa kwenye kasiri lake huku rainibw mbezi beach tumechika na nauli kuja mwenge pls
 
Mfumo wa Serikali tatu hauna ubaya wowote.
na kila mtu awe rais kwenye nchi yake, na pia, kila mtu amiliki ardhi kwao tu, leo mzanzibar anamiliki tanganyika ila mtanganyika hawezi kumiliki zanzibar
 
Maraisi wa Tanganyika na Zanzibar wawe magavana, halafu tuwe na Raisi wa Jamhuri ya muungano vipi hapo?
 
cha muhimu kila mtu ameneji mali za kwenye nchi yake. mali za Tanganyika ziwe managed na WAtanganyika na kupangiliwa na watanganyika, na mali za zanzibar hivyo hivyo.
 
ati mpemba anamiliki ardhi hata kahama, ila mtanganyika akienda kule wanataka aende kwa level sawa na mtaliano na mwingereza, anaenda kama mwekezaji hamiliki kama mtanzania. si ujinga huu? halafu wamejazana bara siku tukigawana mbao watapata hasara kubwa sana na sijui watachagua kua wa wapi, na huku watakuja kwa passport. na uzuri wote sasaivi wapo kwenye database, siku tukigawana mbao ni rahisi tu, unatoa vitambulisho vipya na mtu hawezi kudanganya kwasababu taarifa zake tunazo.
 
Tanzania bado haijapata uhuru nachojua tanganyika ndo ilipata uhuru 1961 na zanzibar 1963
 
Jamaa ameumizwa sana kwasababu tu alitaja Tanganyika. Imagine, tangu enzi Wazanzibar wapo huru kujivunia Zanzibar na kupigania Zanzibar, wana serikali yao, bunge lao, lakini mtu wa Bara akitaja Tanganyika anachokutana nacho ni hatari tupu.

Hutakiwi kujiita mtanganyika, ila wengine wajiite tu wazanzibar. nyerere aliweka uoga wa ajabu sana na bado watu wanaishi kwenye kivuli hicho.

Imefika muda sasa kilichopo mioyoni mwa watanganyika kijadiliwe kwa uwazi na muafaka ufikiwe.

View attachment 2683737
Sio hiyo.

Ile alisema Mfalme atubu dhambi zake. Na akasema yeye ana pesa kuliko serikali
 
Back
Top Bottom