Hii ni Zanzibar ya leo. Sasa Zanzibar watu wa CCM wanahudhuria mikutano ya CUF na watu wa CUF wanahudhuria mikutano ya CCM! Halafu lile toto la tembo linajifanya kushangaa kuona CCM na CUF wanaishi bila ya chuki!
Viva CUF, Viva CCM, Viva Zanzibar.
Tanganyika is next! Tunamuachia Mkwere amalize muda wake halafu Mnyamwezi anakabidhiwa nchi!
Nadhani huyu mama kavaa t shirt ya mafisadi kujisitiri ila kiundani nadhani ni mwana mageuzi wa kweli. Si unajua hizi yebo yebo ukikubali kupokea unapewa na cha juu?
Kumbukeni watu wa tarime walitwambia "Ukipewa fualna, kofia au kanga na CCM, pokea kwa sababu ni kodi zetu. Lakini moyoni unajua nini utafanya". Mimi naishia hapo. Ingawaje mimi siwezi kuvaa nguo yenye alama ya CCM, lakini wale wanaoweza (ambao hawana kinyaa na ufisadi) wanaweza kuvaa lakini wakati wa kura wakampigia Dr. Slaa.