wakuu, hii ya chagua mtu badala ya chama umekaaje?
mwanzoni ilianza kama jambo lisilo serious sana, lakini mpaka sasa tunaambiwa (mwananchi) hata viongozi wa dini wanasisitiza sana kwa mtu kuchaguliwa kwa kigezo cha ubora na si chama(malasusa).
rioba alipata kusema kwamba ccm ikiweka hata ng'ombe atachaguliwa tu; lakini sasa inavyoonekana upepo umeanza kugeuza mwelekeo.
hivi maana yake inaweza kuwa nini wakuu?
Maana yake ni kubwa sana, watu wanatembea kwa kuhonga na kununua watu na wasanii wakuwashangilia tusipo pima uwezo wa mtu twaweza kujikuta tumechagua kelele na kina joti kutuongozea nchi, Tusijali amekuja na ndege ngapi na Bongo flava ngapi Kikwete tunamjua kwa 5 years pamoja na wabunge wengine, Tukubali kubadilika, sasa hivi tunashindwa kutenganisha serikali na chama cha kisiasa, kwani kuna mazoea flani, hata Mkuu wa Police anashindwa kujitofautisha na Chama, Tukianza kuchagua mtu tutajikuta hata viongozi mafisadi wanabadilika kuwa watu wazuei cause wanajua chama hata kitoe vitenge na wax ngapi hakiwezi kumsaidia kupita kama hatatumikia wananchi....
Hata kama unapenda Chdema namna gani, Hata kama unapenda CCM au CAF kwa kiwango gani kama mtu ni mbovu mpotezee....
Huu nimuda wa kuwatumia Viongozi wa kiroho watumie uteule wao kuongea na mtu na kuwafunulia watu ni nani atakae tufaa.. Nashangaa tunawaondoa kwenye uso wa siasa while ni watu muhimu kweli...
Mwakembe kama alifanya vizuri na watu wa jimboni mwake wamerizika bali hwariziki na maamuzi ya Kikwete wampe TIKI Mwakembe na TIKI rais wanaeamini kuwa ataweza kushirikiana na Kikwete....
Nashangaa kwanini tunalaumu Kikwete kumpigia kampeni Lowasa na Chenge ni kwasababu tumeacha kufuata maadili ya mtu tunaendekeza uanachama, CCM imeporomoka kima adili kwa sababu ya uanachama, kuna watu ndani ya CCM wanamchukia Kikwete vibaya Mno ila wako kwenye msafara wake kumpigia kampeni sio kwa sababu ya kupenda kwa sababu ya uchamaaa
Bora kikwete anaenda Kifamilia zaidi, angalia ubora wa familia yake kama vipi chagua yeye