Hii ya DC wa Igunga kuwasaka walanguzi wa sukari mitaani akiwa na migambo imenikumbusha vita vya Kagera

Hii ya DC wa Igunga kuwasaka walanguzi wa sukari mitaani akiwa na migambo imenikumbusha vita vya Kagera

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli hili swala la uhaba wa sukari kama litaendelea tutashuhudia mengi.

Nimemwona Mkuu wa wilaya ya Igunga mh Mwaipopo kupitia Star tv akiwa na lundo la askari polisi waliochanganyika na JW pamoja na migambo wakisaka walanguzi wa sukari mitaani.
Kumbe hii nayo ni vita kama ile ya Corona.

Hakika nimekumbuka madhara ya vita vya Kagera miaka ya 80, walanguzi walisakwa na migambo baada ya miaka 40 msako umeongezewa nguvu kwa kuwajumuisha askari polisi na JW.

Maendeleo hayana vyama!
 
Njia sahihi ya kushusha Bei,flood the market,,
Yaani Supply izidi demand
Mh Hasunga jana ameliambia bunge kwamba kuna tani zaidi ya 20,000 melini zinakuja na tani nyingine 500 kutoka SA zinavuka mpaka wa Kasumulu hivyo tatizo litaisha soon!
 
Kwa umri wangu nilikuwapo Dar es Salaam mwaka 1982-84 wakati wa kipindi cha maduka ya kaya. Hicho ndiyo kipindi tulikuwa tunapanga foleni ya sukari, mchele nk. Mzee Ali Hassan Mwinyi akaingia mwaka 1985 akafanya soko huria la biashara. Kwamba kila mwenye mtaji alete biashara yeyote kwa kufuata sheria.

Ndiyo ikawa mwisho wa maduka ya kaya na kuvaa sulfate badala ya nguo na biashara ya mitumba ikashamiri. Hali iliendelea kuboreshwa kadri miaka ilivyokwenda mbele na BWM naye akapokea kijiti akaendeleza. Naye JK hivyo hivyo akazidi kuifanya Tanzania nchi ambayo ni mahali pazuri pa kuishi.

Huyu JIWE kibwengo wa Kinywarwanda ameturudisha nyuma miaka 50 kutuletea foleni ya sukari. Mwaka 2016 alivuruga kabisa biashara ya sukari kwa kuwaingilia importers na kuwaita mafisadi. Na mwaka 2018 akaharibu biashara ya korosho na mwaka 2020 anashindwa kusimamia ugonjwa wa COVID 19.

Hivi kweli Serkali haina mambo ya muhimu hadi kuanza kufukuzana na wafanya biashara wa sukari? Mara Morogoro kuna foleni ya sukari kwenye maduka ya Abood

Jamani CCM leteni mtu mwingine atawale huyo muacheni Chato awe Rais wa huko. Mbona tayari anayo Airport na traffic lights na sebule ya kuwaapisha kina Mwigulu Nchemba
 
Tunahangaika kulinda viwanda vya ndani ambavyo havilindiki? Watu gani hawa kila wakati ni full excuses tu?

Tena zile zile mwaka kwa mwaka... Ubovu wa mitambo, sijui malighafi!!!! kwa nini tutese mamilioni ya Watanzania kwa Maelf?

Leo nimezunguka na elf 10 sijapata hata robo. Ajabu hapo Zanzibar kilo moja ni sh 2,000 na ipo tele.
 
Mh Hasunga jana ameliambia bunge kwamba kuna tani zaidi ya 20,000 melini zinakuja na tani nyingine 500 kutoka SA zinavuka mpaka wa Kasumulu hivyo tatizo litaisha soon!
Kana wenye viwanda vya sukari ndo wame monopolise kuimport hiyo sukari,tatizo halitoisha
 
Kwa umri wangu nilikuwapo Dar es Salaam mwaka 1982-84 wakati wa kipindi cha maduka ya kaya. Hicho ndiyo kipindi tulikuwa tunapanga foleni ya sukari, mchele nk. Mzee Ali Hassan Mwinyi akaingia mwaka 1985 akafanya soko huria la biashara. Kwamba kila mwenye mtaji alete biashara yeyote kwa kufuata sheria. Ndiyo ikawa mwisho wa maduka ya kaya na kuvaa sulfate badala ya nguo na biashara ya mitumba ikashamiri. Hali iliendelea kuboreshwa kadri miaka ilivyokwenda mbele na BWM naye akapokea kijiti akaendeleza. Naye JK hivyo hivyo akazidi kuifanya Tanzania nchi ambayo ni mahali pazuri pa kuishi. Huyu JIWE kibwengo wa Kinywarwanda ameturudisha nyuma miaka 50 kutuletea foleni ya sukari. Mwaka 2016 alivuruga kabisa biashara ya sukari kwa kuwaingilia importers na kuwaita mafisadi. Na mwaka 2018 akaharibu biashara ya korosho na mwaka 2020 anashindwa kusimamia ugonjwa wa COVID 19

Hivi kweli Serkali haina mambo ya muhimu hadi kuanza kufukuzana na wafanya biashara wa sukari? Mara Morogoro kuna foleni ya sukari kwenye maduka ya Abood

Jamani CCM leteni mtu mwingine atawale huyo muacheni Chato awe Rais wa huko. Mbona tayari anayo Airport na traffic lights na sebule ya kuwaapisha kina Mwigulu Nchemba
Tatizo lako wewe ni chuki. Sukari limekuwa ni tatizo la muda mrefu wala sio kwenye utawa wa JPM tu. Umesahau kwa nini Marehemu Iddi Simba alijiuzuru sababu ya nini?

Kwa ufupi awamu zote kumekuwa na tatizo ambalo linatakiwa kushughulikiwa. Alafu unafanya makosa kumuita mkuu wa nchi kibwengo. Acha lugha za kipuuzi.
 
Tunahangaika kulinda viwanda vya ndani ambavyo havilindiki? Watu gani hawa kila wakati ni full excuses tu? Tena zile zile mwaka kwa mwaka... Ubovu wa mitambo, sijui malighafi!!!! kwa nini tutese mamilioni ya Watanzania kwa Maelf?
Leo nimezunguka na elf 10 sijapata hata robo.... Ajabu hapo Zanzibar kilo moja ni sh 2,000 na ipo tele...
Tulikataa kununua sukari ya zanzibar kile kiwanda cha mahonda ha ha ha ha saizi inakula kwetu sema kwenye hivi viwanda vya sukari kuna hisa za wakubwa ndio mana wanavibeba lakini havibebeki
 
Back
Top Bottom