Silly
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 569
- 180
Ninakunwa kidogo na fikra nazopenda kuziita fupi za viongozi wengine barani Africa. Siku za hivi karibuni ndugu zetu jirani zetu wa Kenya wamepata kushambuliwa na watu wengi kupoteza maisha na katika mashambulizi yote - kikundi cha Alshabab kimetamba kuhusika. Katika masharti yao - Alshabab wanataka Kenya iondoe wanajeshi wake Somalia kitu ambacho viongozi wa Kenya wametoka na kukataa katakata kwamba hawaondoki hadi pale Somalia itakuwa safi.
Hapa majuzi pia Sudan ya Kusini imeingia katika mgogoro wa vita vya wenyewe pande zote zikishikilia kuwa na haki flani flani. Napo pia tumeona viongozi wa Kenya wakijitokeza na kutaka kuisaidia Sudan ili amani ipatikane. Hivi hawa viongozi ambao imekuwa vigumu kwao kuwahakikishia raia wao usalama wa kutembea na kufanya mambo yao kwa amani itakuwa vipi wajihusishe na vita kwa jirani zao wakati kwao nyumba yao inaungua kwa mashambulizi ya magaidi na wahalifu wa ndani.
Na ni vpi yule mpiga kura aliyewapa kazi hao jamaa ataweza kusikika..naomba mwenye kuelewa diplomasia anifafanulie ili nipate elewa.