Hii ya Singida Big Stars Kuwapokonya Simba SC Mchezaji Imekaaje?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Walianza Berkane. Wakafanya umafia wao kwa Adebayor.

Wakafuata Yanga SC. Wakafanya umafia wao Kwa Aziz KI.

Akaja Rais wa Vipers SC akafanikiwa kuwabania Ceaser Nzoki. Hata ikawafanya waende Nigeria kum’beba OKRAH.

Kocha Stuart naye amewakataa kwa kigezo cha kushindwa kumuweka wazi kiasi cha bajeti ya usajili cha klabu kwa dirisha hili.

Nasikia hata huyo Sylla wa Horoya nae huenda wakamkosa kwa sababu wako kwenye ushindani na kigogo mmoja wa kaskazini huko.

Leo hii nao watoto wadogo wa mjini aka walima Alizeti wamefanikiwa kuingilia kati mazungumzo ya Habibu Kyombo na kufanikisha usajili wake.

Inasemekana kuwa Simba SC walikuwa wanapanga kumpa mchezaji huyo dau dogo kwakuwa alikuwa free agent na pili hakuwa akihitajika na timu nyingine kubwa ya hapa nchini.

Hizo taarifa zikasambaa si tu miongoni mwa watu wa karibu na Kyombo bali pia hata zikamfikia yule Mbunge aliyemsajilisha Fei Toto pale Singida United (Enzi hizo).

Huyo bwana baada ya kupata taarifa hizo akapandisha dau nono kwa mchezaji kama signing fee yake pia akamuahidi mshahara mnono ambao Simba SC hawakuwa tayari kumlipa.

Dogo akatamanika na akizingatia ana vina saba na U’yanga akaona asihangaike kwenda kuichezea timu ambayo hana mapenzi nayo ya dhati kutoka moyoni kwa ujira mdogo.

Msimu huu hawa jamaa wamechanganyikiwa mno.

Siamini na wala sitaki kuamini ninachoona kinaendelea kwenye kambi yao.
 
Tatizo kila timu hapa bongo inatumia brand ya Simba kutafutia kiki ili nayo ipate kuzungumziwa

Huu mchezo ulianza na Yanga, wanatengeneza drama kuwaaminisha mashabiki zao kuwa mchezaji fulani Simba inamnyatia kumsajili ili wao Yanga wakimsajili mashabiki wafurahi kuwa wamewazidi kete Simba

Sasa na hizi timu zingine zikiona hili jambo nazo zinajikuta zinafata mkumbo
 
Leo hii nao watoto wadogo wa mjini aka walima Alizeti wamefanikiwa kuingilia kati mazungumzo ya Habibu Kyombo na kufanikisha usajili wake.

Soma hii yote halafu useme ni nani amempora mwenzake mchezaji: Singida amempora Simba au Simba amempora Singida:

Kiongozi wa juu na mwenye maamuzi ndani ya Singida amesema hatukuwa na nia ya kumtambulisha Kyombo leo wala mchezaji yoyote yule hadi hapo msimu utakapo malizika.

“Tumeamua kumtambulisha Kyombo kutokana na kupata taarifa za uhakika kuwa Simba imemsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili ili hali huku nyuma akiwa amechukua cha kwetu tayari,” amesema Kiongozi huyo na kuongeza;

“Kama Simba itakuwa tayari kutupatia kiasi cha Sh35 milioni ambacho tulimpatia Kyombo tunaweza kukaa nao meza moja kwa ustaarabu na tukawaachia mchezaji aende kucheza kwao,”

“Jambo kama hili limewahi kutukuta Singida wakati wa nyuma kwa Feisal Salum tulimsajili ila mwisho wa siku tulikubaliana na Yanga walitupatia gharama zetu na akaenda kucheza kwao na yupo huko hadi sasa."

“Ila tumefanya utambulisho wa Kyombo leo baada ya kufahamu Simba imemsaini tayari mkataba wa miaka miwili wakati hapo awali alianza kusaini kwetu Singida nahisi kuna watu walimshauri vibaya, ila kwetu tulimpatia pesa hiyo na alishatumia kwenda kufanya mambo yake.”
 
Jambo kama hili limewahi kutukuta Singida wakati wa nyuma kwa Feisal Salum tulimsajili ila mwisho wa siku tulikubaliana na Yanga walitupatia gharama zetu na akaenda kucheza kwao na yupo huko hadi sasa...
ile timu iliyoshuka daraja ndio hii? hapa mbona kama kuna timu a na timu b zote za tajili mmoja alafu....
 
Singida ya Mwigulu, sasa sijajua unamaanisha kama na Simba ni ya Mwigulu pia au la
singida united alisajiliwa fei toto akapelekwa yanga
hii singida mpya kasajiliwa kayombo

wamefanya reference ya walicho wahi kukifanya huko nyuma kuwa patia yanga fei toto hivyo hata simba kwa singida hii wata wapa kayombo ila kwa shart...

sasa swali singida hii na singida ile ni timu a na b na mmiliki ni mmoja? itakuwaje zikicheza ligi moja?

usije toa mifano ya timu za majeshi au kurugenzi au rtc etc...
 
sasa swali singida hii na singida ile ni timu a na b na mmiliki ni mmoja? itakuwaje zikicheza ligi moja?
Hakuna Singida mbili kwenye ligi moja. Singida ya mwanzo iliporomoka maana ilikuwa kwa ajili ya kampeni za urais. Singida hii imeanzishwa kwa kununuliwa kutoka DTB, nayo ni kwa ajili ya kampeni za urais ujao. Lakini kujibu swali lako, hakuna Singida mbili katika ligi moja
 
Kumbe
 
Kwamba Kyombo ndio amesababisha uanzishe uzi? [emoji16]

Sio Kyombo.

Ni kitendo cha Singida Big Stars kuwapokonya Mchezaji mliokuwa naye katika mazungumzo. [emoji23]
 
Soma hii yote halafu useme ni nani amempora mwenzake mchezaji: Singida amempora Simba au Simba amempora Singida...

Usiwasikilize hao wewe...!

Nisikilize mimi ambaye niko kwenye eneo husika la kupata taarifa za ndani.
 
soma alicho andika... hizi timu zipo na zinashiriki ligi za tff na bodi zake, kuna uwezekano wa siku moja kucheza ligi moja...
 
Ni mapema sana kusema lolote kuhusiana na usajili mpaka mwisho wa mwezi huu kila kitu kitakuwa wazi kwani kurwa na doto wa Kariakoo watakuwa wameshapeleka majina ya awali ya usajili wao CAF. Kwenye usajili dakika moja ni kubwa sana kumbuka Hamis Tambwe alitemwa mida mibaya sana na Simba Yanga wakambeba sekunde kadhaa kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Na ikifika wakati wa usajili hapo bongo kuanzia mitandaoni, redioni, kwenye TV na magazetini ukisoma na ukisikiliza halafu ukaamini kwa kweli lazima utachanganyikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…