Hii ya Sugu ya mwaka 1996 ni hatari

We kweli miss moro..ya dar tuachie wenyewe
Mkuu inaelekea unafahamu mengi kuhusu muziki wa kizazi kipya enzi unaasisiwa kwa faida ya wengi ungeshusha nondo zaidi kuhusu wasanii wa kipindi hicho na media apearence zao kwanye tv na redio
 
Sugu noma saana hua ana nipa sababu ya kupambana na maisha hasa nikisoma kitabu chake cha from street to the parliament
 
sugu ni noma nakubali hip hop yake tokea kitambo.
 
"Nimesimama...akili inanituma kusema nimesimama nisikilize nnachosema...nimesima"×2
Kwako maisha ni matamu
kwetu ni magumu ndomana tunalaumu
vita inayoendelea kati ya polisi na machinga wengi tunapinga
Kivipi mi nirudi kijijini
Wakati mbunge wangu yupo mjini
Anatanua na shangingi
Ni nna akili nyingi toka msingi
mpaka sekondari
ila niliona hatari
kwenda chuo kikuu
naogopa FFU watanivunja miguu
nitakapogoma kusoma
mi nasema ili msijesema mi sikusema
chochote nnachofanya kwa nchi yangu kiwe chema
siku za nyuma baba alisema
dunia tambara bovu
itakubidi uwe shupavu
wapo watakaokuona ni mpumbavu
na wapo wataokuona ni mwerevu
maisha ndivyo yalivyo kila kitu ovyoovyo
kampeni za uchaguzi zaambatana na matusi sijapata kusikia
ni demokrasia au ghasia aaah

Nna hasira na nchi yangu mi ni mbongo mwenye usongo
naanzisha songombingo
nabeba bango
watu msiniite mtukutu
Nitakaposimama na kusema nimesimama"

Hii flow haijawahi kubadilika miaka mingi tangu way back.Much respect kwako mheshimiwa Sugu.A true and real activist
 
Hip-hop ni maisha, Hip Hop inaishi
 


HipHop lives. HipHop is always for community potentials.

Mwanaharakati Sugu on air since back in deyz kitambo, kabla ya ujio wa FM radio.

-Kaveli-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…