Hii Yaweza Kuwa Fursa Kwa wana JF

Hii Yaweza Kuwa Fursa Kwa wana JF

Kafiti

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
537
Reaction score
220
Habari Wanajukwaa,

Nimeiona hii fursa nikaona ni vyema kushare nanyi, yeyote mwenye uhitaji wa kufungua biashara eneo hili nafasi hii hapa.

Nyumba ilitengenezwa kwa ajiri ya shughuli za mgahawa(cafeteria) ila shughuli zake zimesitishwa baada ya aliyekuwa mmiliki kuhama. Nimekuwa nikila mgahawa huo na nimeshtushwa na kufungwa kwake ila uondokaji wa mtoa huduma eneo hilo unaliacha hilo eneo wazi kabisa kwa ajiri ya biashara zingine ama ileile ya mwanzo.
Biashara niliyoifikiria ni ya ufundishaji wa course za computer(level ya certificate) na utoaji wa huduma hizo.

Nimetembelea maeneo hayo mara kwa mara na maeneo ya karibu na eneo hili Yombo, Buza. Na kwa haraka tu nikagundua eneo lote ya Yombo watu hawana hii huduma ya ufundishwaji wa computer. Na eneo hili liko barabarani kabisa hivyo litaweza kuvutia wanafunzi wengi wa maeneo ya Yombo, Mbagala , Tandika , Jet , Kitunda na maeneo ya jirani.

Muonekano wake wa ndani ni mzuri na wa kuvutia kwa kufundishia. Kuna faida fulani kwa mtu atakaye wahi mapema maana anayefunga anaviti na meza ambazo unaweza kuongea naye na kuvitumia kwa maana anahamia eneo la mbali na hapo.
Mwenye eneo anahitaji 150,000/= kwa mwezi naamini unaweza kuongea naye kidogo.

Nimewasilisha wazo langu kama kuna aliyefikiria kuanzisha kitu kama hiki huu ni msaada pia. Kama unataka kufungua biashara nyingine kwenye eneo lile naweza kukusaidia pia kuwasiliana na mwenye eneo.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom