Miongoni mwa wabunge waliopata umaarufu katika Bunge la mwaka 2015 - 2020, ni Selemani Bungala, maarufu kama Bwege, aliyekuwa mbunge wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kutangaza kuhamia ACT Wazalendo baada ya Bunge kuvunjwa.
Mwananchi imefanya mahojiano maalumu na mbunge huyu wa zamani ambaye amezungumzia mambo tofauti, ikiwemo siasa za upinzani, maisha yake baada ya kukatwa mguu na mtazamo wake kwenye siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Bwege anasema upinzani hauwezi kukishinda Chama cha Mapinduzi (CCM) bila wao kuungana ili kuwa na nguvu ya kukabiliana na chama hicho tawala ambacho kina nguvu kubwa ya kifedha, mamlaka na mtaji wa watu. Anapendekeza asimamishwe mgombea mmoja atakayeungwa mkono na vyama vyote vya siasa.
Chanzo: Mwananchi