KERO Hiki kinachoendelea usaili wa kuandika ni ubatili mtupu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kulingana usaili unaoendelea wa idara ya Afya kupitia PSPR mikoani.

Kumekuwa na hali isiyo ya uwazi katika kutenda haki ili kupata wasailiwa wenye vigezo vya kuajiriwa.

Kwanza katika mchakato wa ufanyaji mtihani wa usaili hakuna maelezo yakueleweka toka PSPR ni kiwango gani cha ufaulu wa marks kinatakiwa ili mtahiniwa awe amefaulu kwenda hatua inayofuata

Kwani baadhi wamekuwa selected kwa ufaulu wa 58, 71, 82, na 86.

Kwakuwa wanahitaji ushindani ni vema wabainishe ni kiwango kipi cha ufaulu wanakihitaji.

 
Relax ufaulu wa kada husika huchukuliwa kutokana na idadi ya nafasi za kazi zilizopo ivo wale the best ndio huwa wanachaguliwa Na nafasi moja inashindaniwa na watu watatu

Soma sana psrs upiti kindezi pole kwa mkando jipange upya

Hii nzuri kazi iendelee
 
Nilikuwa sijui hii kwahiyo kama nafasi ziko 100 watu tuko 50 ata nikipat 20 naweza nikapita
 
Kwa nilivyofatilia hizo selected za psrs ni Huwa wanaaza kukata kuanzia 50 kwenda juu kinachotokea ni kuwa unaweza kupata 50 usichaguliwe inatokana na ratio kwakuangalia nafasi pamoja na idadi
 
Nadhani umecoment hata bila kusoma, jaribu tena kupitia hayo matokeo kuna watu wana 84 and they were not selected lakini wenye 71 wako selected. YUPI ndezi kati huyu mwenye 84 na 71????
 
Issue ni pass mark siyo groups, labda unambie ni miaka tofauti
Jiongeze, kuna kada mtu wa kwanza ana 99 na kuna kada nyingine wa kwanza ana 70 kwahiyo wasimchukue engineer aliopata 70 kwasababu kuna daktari kapata 99? Huu sio mtihani wa la saba kwamba wote wako sawa...kila kada inatreatiwa differently kutokana na ufauli na ndio maana zikiwa chini ya 50 hawatachagua hata mmoja nafasi zinatangazwa upya (Readvertised)
 
Wewe hujaelewa pamoja na mtoa post kuweka ushahidi.
 
Wewe hujaelewa pamoja na mtoa post kuweka ushahidi.
Jamaa ameandika sahihi, ila kama ww n mgeni wa psrs bc huwezi kumuelewa.
Issue ni pass mark siyo groups, labda unambie ni miaka tofauti
Kitu kama hujui uwe unauliza mkuu, acha kukaza kichwa. Hizo n post mbili tofauti.
Nilikuwa sijui hii kwahiyo kama nafasi ziko 100 watu tuko 50 ata nikipat 20 naweza nikapita
Pass inaanza na 50% hata wakihitajika 10 halafu mko wa5 na ww umepata hy 20 huwezi kupita.
Pitia mada ya 'kwann utumishi wanachelewa kuita watu kazini' ili ujifunze na uache kulalamika hovyo.
 
Well said 🤝
 
Pole mkuu hiyo ni kama ligi ya england point sawa ila kombe linaenda kwa man city eti kisa magoli ni uhuni unaochekesha
 
Soma vizuri alichoaandika
 
Hawa majamaa wamekutana na mikando wanakuja lia lia humu jipangeni mwakani mtatoboa
 
Hawa majamaa wamekutana na mikando wanakuja lia lia humu jipangeni mwakani mtatoboa
Hakika kwenye haya maisha lazima ukubali kuna watu wanajua zaidi yako, na the good way to beat them nikujiandaa na nakujinoa uwe bora kama wao, na sio kuatack system! speaking from experience, nafasi ya kazi unakuta anahitajika mtu mmoja mnaunga group la kusaidiana unagundua kuna wanyama wawili watatu kwenye hilo group ni nondo vibaya mno na usitoshe wana experience, sasa hapo ni nini ? kujifunza na kujipanga for the next time.
 
Wakati nikiwa Kijana nilifanya sana interview nikawa naliwa kichwa ila baada ya kujua sababu Interview moja tu nilitoboa hivo ukiona umeshindwa sehemu hebu jiulize nini kimetokea kwann yule kafaulu na mm nimefail jiulize kwa hapo na jipange sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…