Hiki kitu kimeniumiza sana!

brave_3

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
1,186
Reaction score
705
nilipita mchana mkowa wa TABORA wilaya ya IGUNGA . kuna tatizo la mgomo wa walimu . walimu wanadai mishahara ya miezi miwili . cha kushangaza ni kwamba halmashauri ya IGUNGA inasema itawalipa lakimoja kwa ajili ya kujikimu. da hii kitu imeniuma japo mimi sio mwalimu . unakuta mwalimu kapanga, chakula hajanunua na bado matumizi madogo madogo. hivi kwa hali hii elimu tanzania itakuwa kweli. ifike kipindi nayo serikali iwa angalie walimu kwa jicho la kwanza. POLENI WALIMU
 
Inamaana wanalipwa kimikoa?? Au walimu wote hawajalipwa? Au mishahara kwa miezi gani?
 
walimu nao misimamo hawana ati!

chama wanalo lakini naona wameshikwa kote kote.
 
Izi ajira za serikali izi..mshahara ulioutolea jasho unakua ka msaada vile
 
Sema walimu wa huko, usiseme walimu wote, kuna walimu tunajitambua mno
 
Sema walimu wa huko, usiseme walimu wote, kuna walimu tunajitambua mno

Acha uongo, mpaka leo jiulize cwt inakusaidia nn? Unakatwa sh ngap kwa cwt? Ni halali? Haya, katibu mkuu alitoa waraka wa re categorization, unaufahamu? Umenufaikaje? Unajua mshahara wa rais wa cwt? Ni haki? Ok, perdm huwa unalipwa sh ngapi? Ni halali? Mpaka leo umeenda lkizo mara ngapi? Umelipwa mara ngapi na sh ngapi?, ni halali? Ni haki yako kuwa na likizo ya 30 days annually, umeenda mara ngapi,? Jipime ndo ujiulize kama unajitambua au la. CCM NI MBAYA SANA, WANAWATUPA WALIMU MPAKA IFIKIE UCHAGUZI, AMKENI NDUGU, HII NI HAKI YENU KUDAI MSHAHARA, KUMBUKA, NGUVU YA MNYONGE NI KELELE
 
Inamaana wanalipwa kimikoa?? Au walimu wote hawajalipwa? Au mishahara kwa miezi gani?[/QUOTEkwa huku hata sijui tatizo ni nini badala walipwe bali halmashauri inawambia wakopeshwe laki moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…