Hiki ndicho hutokea rohoni baada ya mtu kufa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Hakuna aliyewahi kufa akarudi akasimulia yanayoendelea Kwenye roho baada ya kufa.ila mimi Nimekaa nikazichunguza kweli za kimaandiko nikatambua hali tunayokuwa nayo baada ya kufa na Sasa nawashirikisha.
Kwanza stories yenyewe inaanzia Kwenye Ile process ya mwili kutaka kujishut down.mwili(body) Ni Kama simu,nafsi(soul) ni Kama line,uhai(life) Ni Kama chaji,roho(Spirit) Ni Kama network (mtandao).na mmiliki wa mtandao Ni MUNGU na ndo maana hata hapa ulimwengu hizi tigo,Vodacom Zina wamiliki wake so hata MUNGU ndiye anayemiliki kuanzia roho,mwili mpaka uhai tulionao Sasa baada ya kujua yote hayo turudi Kwenye process ya mwili kuzimika yaani kufa.
Ipo hivi tunajua simu ikiwa Haina chaji utaona Kama inakuletea warning kuwa muda sio mrefu itajizima.hata kwenye kufa dakika za mwisho mwili utakuwa unahangaika zile organs kukata mawasiliano.muhusika anayefariki atajua kabisa kuwa amebakisha dakika chache Sana.
Wote lazima tuhisi maumivu dakika ambayo roho itakuwa ikitoka hata Kama mnakumbuka yesu alilia kuwa roho ipo radhi Ila mwili Ni dhaifu.ni Kama vile umebanwa pua na mdomo usiheme.mtu anapokaribia kufa au mwili kujitenga na roho anapatwa na hali gani?

1. Miguu kuishiwa nguvu na kushindwa kutembea inakamatwa na Ganzi (Mf. Mwangalie Kuku na wanyama walioumwa hadi kufa miguu huwa haifanyi kazi tena) hii pia ni hadi kwa Wanadamu tu. Na kuanza kupatwa na ubardi

2. Ganzi huwa inaanza kutembea mwili mzima na unaisikia kabisa

3. Sehemu za mwili zinaanza kupatwa na ubaridi mkali kila sehemu

4. Viungo vya mwili hasa mikono huwa inafanya involuntary movement yaani vinaanza kunyooka hasa hiki jirani na kidole gumba

5. Kuanza kuona giza yaani mfano wa kufumba macho wakati macho yako yapo wazi

6. Kukata Kauli wengi wanasemaga mwanadamu anapokaribia kufa hufikia hawezi kuongea tena ila ganzi inakuwa katika mdomo hasa ulimi kwahiyo hunapoteza uwezo wa kutamka kabisa

7. Taarifa inayofika wakati huo (si ya woga au kusema ni uwoga) unafahamu kabisa sasa ndio ninakufa hakuna kinajojificha kabisa.

8. Sehemu inayobakia yenye joto ni kifuani tu (huwa najiuliza sana ktk saikolojia niliwahi soma siku za nyuma nafsi ya mtu inaishi katika ubongo wa mbele) lakini to that moment kifuani ndio panakuwa pana struggle sana huku ganzi ikipambana kufikia hapo lakini katika logic ya kawaida sababu ya moyo hupo hapo ukipatwa na ganzi inamaana shughuli zote za mwili zinasimama rasmi

9. Namna mwili unapokuwa unapambana kutafuta joto ndipo kuna movement flani huwa inaufanya ambao watu waliofariki wanajikuta miili yao inakaa kwa namna flani au kama kukakamaa. (mfano mmoja Angalia wanaokufa maji)

10. Kufika point hiyo ulimwengu wa kuota unaamia katika uhalisia unakuwa ni kama unayeota katika fikra lakini hupo hai unaona kabisa na fikra yako inafanya mrejesho kwa haraka haraka kuhusu maisha yako hadi hapo ulipofikia halafu unajiuliza ulikamirisha wito wako? Au nini umefanya muhimu kwa muda wako wote ulioishi duniani (Wito) Tafsiri nyepesi hakuna mwanadamu anayezaliwa bure hapa au yupo yupo tu. Kila mwanadamu anakazi maalum anaifanya awe Mwanajeshi, Mwalimu, Nesi, Daktari, kufanya biashara Fundi au taaluma yoyote ukiacha tu zile za uchungaji, upadri ua za dini nk ambazo wengi udhani ndio za kumtumikia Mungu.

Sasa Na hata baada ya kifo huwa Kuna Jambo linafuata Sasa kuhusiana na roho. tofauti ya Jambo Hilo inaonekana huwa inakuja baina ya mtu anayetenda maovu na yule aliyekuwa anafanya mazuri.
Hili Ni Kama fumbo Sasa ili twende sawa ndugu msomaji Hapo ulipo fumba macho Kwa sekunde tano.nadhani umeona kinachoendelea ubongoni Sasa kile kinachoendelea ndi o roho yenyewe.sasa Aliyefanya madhambi na hakutubu yeye Ile roho yake huwa inahangaika Sana Ni kama vile utembee usiku ndani ya nyumba gizani utakuwa unapamia pamia vitu ndivyo ilivyo kwa roho ya mtenda dhambi.itateseka kwa style hio.
Ila kwa yule muadilifu yeye roho ikitoka hisia ambazo roho itakuwa nazo nazifananisha na mtu aliyelala usingizi mtamu.
Kwa hiyo hakuna Cha mbinguni Wala motoni isipokuwa we fanya mema na ibada ili ukifa mema yako roho yako ikikumbuka itaamua kutulia yenyewe kwa kuwa at that moment utakuwa huna mamlaka na roho yako.itakuwa inafanya kazi yenyewe jinsi ipendavyo.ila ukifanya mabaya na madhambi roho yako itakuwa haijatulia itakuwa inatamani kurudi kwenye mwili ili ifanye mema lakini itashindikana na kule kushindikana ndio tunakufananisha na jehanam.lakini kiukweli hakuna jehanam Wala hakuna kwenda mbinguni.. paradiso ipo hapa duniani yaani hapa ndipo penyewe na dunia Haina mwisho itaendelea kuzunguka hivihivi mpaka wakati usio na kipimo.humu duniani waadilifu wataishi milele na wale waovu watapotezwa milele wasionekane Tena!
 
Mtoa mada ukifa naomba uje uthibitishe ulichoandika.
 
Umeanza vizuri umemaliza vibaya.
Sasa Mwenye mtandao anaweza akashindwa kuzihifadhi line zake mwenyewe?
Mungu atashindwa kuipangia mahali pa kwenda roho imtokayo mwanadamu,kiasi cha kuiacha izagae hobelahobela duniani?
 
Aliyemaliza kusoma jamani naomba uniambie
 
Baada ya kufa roho inakuwa inazurura tuu na inakuwa katika hali ya uzezeta, inatafsiri vitu kinyume, inaona lakini haina mawasiliano ya kawaida, haina uwezo wa kumtambua mtu
 
Mada kama hizi zinahitaji roho mtakatifu akushukie ili uichambue vyema,

Back soon, kuendelea
 
Heaven & Hell is a very big secret and an imaginary state bonded within a human subconscious mind of many people. To be honest all of us know nothing concerning this. Let's pray endlessly and keep doing good things but most important of all is to be loving each other relentlessly until the end of time. And that's what God wants from us.
 
Baada ya kumaliza kusoma ikabidi nimuangalie muandishi ni nani...daah
 
Hapo chini umeandika vizuri mkuu.Naomba ujumbe huu umfikie Jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa ujawai kufa maana yake unatudanganya..Unasema mtu akikata roho anapata maumivu kuna wengine wanakufa huku wanakula raha wengine wanacheka Yesu alipata maumivu misumari sio mchezo au mwizi anayechomwa moto tofauti na wengine wanakufa huku anafanya mapenzi
 
URE TOTALLY WRONG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…