Hiki ndicho Mchawi anamzidi Mkristo asiyeamini hivi

Hiki ndicho Mchawi anamzidi Mkristo asiyeamini hivi

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Tofauti ya mkristo na mwanasayansi. Mwanasayansi anapoishia mkristo ndipo anaishia.

Kuwa mkristo ni kuamini unauwezo wa kuongea na kuvielekeza hata vitu visibyoongea na vikatii. Katika sayansi hiki kitu hakipo. Ikiwa unaamini Biblia na huamini haya, imani yako iko chini kuliko imani ya wachawi na majini kwa shetani wao.

Mchawi anaweza kumuamrisha Paka, Mbwa, Akaongea na ardhi, vumbi, miti na akaifanya ifanye anavyotaka.

Ikiwa unamuaminj Yesu alafu huamini kuwa hata mawe au nyumba au gari ukiongea nalo linakusikia. Watu wabaya wanaongea navyo vikudhuru wewe.

Ikiwa unaamini utakuwa na uwezo wa kugeuza na vikawa silaha zako za kumshindia shetani. Hata Moyo, figo, magonjwa wako unaweza kuongea nayo.

Ushahidi.
Yesu aliongea na upepo
Muda aliongea na mawe.
Yesu aliongea na homa.
Baalam aliongea na punda.
Ardhi ilimlilia kaini.
Nabii kijana aliongea na madhabau (Mawe kuni).
Biblia inasema anga linaongea. Latangaza utukufu wa Mungu .

Musa aligeuza vumbi likawa chawa.

Yesu hakutania aliposema.
Unaweza kuuambia Mlima, mkuyu ukafanya unavyotaka.

Hii ni siri kubwa. Hata magonjwa unaopoongea nayo, kama yameletwa na majini hayo majini yatapiga kelele na kuondoka. Mfano Juzi mama mmoja aliniambia anaumwa kisukari cha ghafla. Nikaanza kuongea na kisukari na kukiambia kitoke ghafla akaanza kupiga kelele. Kumbe ni tujini tumesurbotage insulin. Akawa mzima.

Ila hata kama ni cha kibaiolojia unaongea nacho. Acha watu wakuone umechizi ila Mungu anakuelewa. Kitatii na kuondoka ikiwa roho ataona vyema. Ila kumbuka wengi Mungu hatawaponya kwa sababu wanafanya kusudi kujiletea magonjwa hata kama waikipona mfumo wao wa maisha utayaleta tena. Hata usijisumbue. Wafundishe badala ya kuwachosha na maombi.


Kama umepata kitu sema amina.
 
Kama ni mkristo na huamini unaweza kuongea na vitu visivyoongea vikatii na kukusaidia. Wachawi na mashetani wanaamini na wanatumia kukudhuru.

Acha dini za kibailojia. Anza kumuamini Mungu kibailojia na kiroho (Beyond physical nature/Realm).

Kuna mtu anachukua unyayo wako, au Uzi kwenye gauni lako LA arusi anautamkia maovu na yanakupata. We we ukikaa kimya utaendelea kuumia.

Jua jinsi ya kutumia kinywa kikusaidie kibailojia na kiroho.

Ukielewa usisite kusema Amina kwa Bwana.
 
Mchawi anaweza akamshinda Mkristo na Mkristo anaweza akamshinda mchawi. Hapa inategemea na nguvu ya imani, mwenye imani zaidi atamshinda mwenzake.
 
Hiyo ni dhana hizi story hazinaga evidence ndio maana ushirikina unaaminika sana kuliko kitu mambo ya Yesu miujiza,
 
Mkuu hebu uwambie mlima mbeya uje dar apo nami nitasadiki uyasemayo ukishindwa ni pumba na porojo kama zingine.
 
Mkuu hebu uwambie mlima mbeya uje dar apo nami nitasadiki uyasemayo ukishindwa ni pumba na porojo kama zingine.
Kama kuna sababu ya wenyewe kuja Dar unakuja.
Ila kama ni mashindano tu hauji.

Ukisema haiwezekani inamaanisha Mungu wako ni dhaifu ameweza kusimamia trillions za sayari kuzunguka katika universe ashindwe kuhamisha kamlima rungwe ambako kapo katika sayari dunia ambayo ni kama punje ya mchanga katika bahari ya universe.

Suala sio Mimi kufanya suala ni Mungu kufanya kupitia Mimi chochote atakacho kwa utukufu wake.

Inawezekana ila sio kwa mashindano Bali mapenzi na utukufu wa Mungu.
 
Hiyo ni dhana hizi story hazinaga evidence ndio maana ushirikina unaaminika sana kuliko kitu mambo ya Yesu miujiza,
Unaamini miujiza ya wachawi kuliko uwezo wa Mungu.

Kama unaweza kulala ndani, mchawi akaingia ndani bila kufungua mlango akakuchanja chale na kukunyoa nywele.

Sasa ni makosa kuamini wewe ikiwa na Mungu unaweza kufanya zaidi ya huyo mdau.

Shida ni ufahama na maarifa tu. Sio nadharia.
 
Tatizo kwanini hatuwezi kufunguka maana tunajiona tuna haki(Umeiba ukaenda kujenga Mara sukari ikakupata ulipaswa kuomba toba kwanza maana ulisha kosa .
 
Ukutoa sadaka ipasavo jua utapigwa Magonjwa utazipeleka hosipitali hizo Pesa.He tutapataje kupona?
 
Back
Top Bottom