real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,299
Kutotibu malaria wakati wa ujauzito, matumizi ya vyakula na vinywaji visivyo salama hasa vyenye gesi na tindikali ni chanzo cha kuzaa watoto wenye maumbile yasiyo ya kawaida ikiwemo mapacha walioungana
Vitu hivyo vimetajwa kuwa sababu ambazo huvuruga mfumo wa utengenezwaji wa viungo kipindi ambacho mtoto huanza kukua tumboni
Hayo yalisemwa jana na daktari bingwa wa upasuaji wa watoto kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Zaituni Bokhari alipokuwa akitoa majibu ya vipimo vya mapacha wa kike walioungana waliozaliwa hivi karibuni mkoani Morogoro
Dk Bokhari alisema hakuna sababu maalum mpaka sasa ila kuna vitu ambavyo husababisha kujifungua mtoto ambaye sio wa kawaida
Chanzo: Mwananchi