CompaQ
JF-Expert Member
- Dec 31, 2012
- 281
- 134
Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani katika kupambana na ugonjwa wa malaria pia kuhamasisha uelewa ili kukabiliana na ugonjwa huu unaoongoza kwa kuua watu wengi.
Wataalamu wa afya wanaelezea uogonjwa wa malaria kuwa ni tishio kwa mama mjamzito na mtoto aliye bado kuzaliwa.
Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba mwaka 2012, malaria ilisababisha vifo vya watu 672,000 duniani.
Utafiti huo unaonyesha kuwa viofo vingi ni vywa watoto na wengi ni wa Bara la Afrika.
Takwimu zinaonyesha kuwa kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja hufariki dunia Barani Afrika.
Hapa nchini inakadiriwa kuwa kila mwaka malaria husababisha vifo vya watu zaidi ya 60,000.
Karibu aslimia 90 ya malaria inayopatikana hapa nchini ni ile isababishwayo na vimelea vya malaria aina ya plasimodium falciparum.
Aina hii ni hatari na husababisha madhara kuliko aina zingine za malaria.
Miongoni mwa madhara hayo ni kama upungufu wa damu, malaria yakupanda kichwani na madhara katika mfumo wa hewa na sukari kushuka.
Ni jambo la kawaida ugonjwa huu kuwapata wajawazito mara kwa mara kipindi cha kulea mimba kutokana na mabadiliko ya kimwili.
Uwepo wa mabadiliko haya ni mahususi na ni faida kwa maendeleo ya mtoto aliye bado kuzaliwa.
Kwa upande mwingine mabadiliko haya yanamuweka katika hatari ya kuugua malaria kirahisi ukilinganisha na wale wasio wajawazito.
Tanzania ni moja ya nchi zilizopiga hatua katika kutimiza malengo ya milenia na kufanikiwa kulifikia lengo kwa kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano.
Mafanikio hayo yanatokana na juhudi za Serikali kupunguza vifo vya watoto katika mikoa mbalimbali hususani ile sugu kama vile Geita, Kigoma na Lindi.
Tishio kwa wajawazito
Kama nilivyoeleza, mabadiliko ya mwili yanayotokana na kipindi cha ujauzito, madhara yake yanachochea magonjwa mengine na ulio hatari zaidi ni malaria.
Mabadiliko hayo pamoja na uangalifu wa kitiba unaopaswa kuchukuliwa ili kulinda afya ya mimba, wataalamu wengi wa afya hupata wakati mgumu katika kutibu malaria kwa mjamzito.
Jambo la kuzingatiwa pia ni kwamba mabadiliko ya kipindi cha ujauzito huambatana na hali inayomfanya mama kuwa katika hatari ya kupata madhara makubwa pindi anapougua malaria.
Mabadiliko hayo huandamana na hushuka kwa kiwango cha kinga za mwili.
Hii ni kwasababu kinga ikiwa juu inaweza kuharibu mimba kwa kudhani mimba ni adui kwakuwa nikitu kigeni mwilini. Lakini kushuka huku kwa kinga ni faida kwa vijidudu vya malaria kwani huweza kumnasa mjamzito kirahisi na kumdhuru.
Ikumbukwe pia kila tupatapo maambukizi mbalimbali, mwili hujitengezea ulinzi kujihami dhidi ya ugonjwa
Kwa upande wa malaria mwili hutengeneza kinga ingawa sio kamili inayoweza kuzuia vijidudu vya malaria kwa asilimia 100.
Mjamzito anayekulia maeneo yenye mbu hukosa hicho kiasi kidogo cha kinga na huku yule ambae anabeba mimba kwa mara ya kwanza, kinga yake ya mwili inakuwa haina uzoefu na uvamizi wa vijidudu wa malaria ukilanganisha na yule mzoefu.
Mabadiliko mengine ya kipindi cha ujauzito kama vile kutapika, kuchefuchefu na hali ya kutopenda kula humfanya mjamzito kutokuwa na lishe nzuri hivyo kutokuwa na kinga imara.
Madhara mengine ni upungufu wa damu na mbaya zaidi ni kwamba hali hiyo huchochewa na kuwa ya kiwango kikubwa zaidi mama ashambuliwapo na malaria.
Pale malaria inapokuwa imeambatana na upungufu wa damu huweza kuambatana na madhara makubwa kwa mtoto ambae bado kuzaliwa.
Madhara yanayoambatana na hali hii ni kama vile mimba kutoka, mimba kuharibika, mtoto kutokuwa na ukuaji mzuri, kuzaliwa kabla ya mda kutimia, kuzaliwa na uzito mdogo, kichanga kuishiwa nguvu, kufia tumboni au kuzaliwa na malaria.
Kwa upande wa mjamzito huambatana na madhara kama vile upungufu mkubwa wa damu, malaria kupanda kichwani.
Uwepo wa vijidudu vingi kupita kiasi mwilini mwa mama pamoja na sumu inayosababishwa kwenye mfumo wa damu, figo kushindwa kufanya kazi, chembe hai nyekundundu kuvunjwa kupita kiasi, kukojoa mkojo mweusi au kawahia.
Hizo ni ishara ya mwili kudhurika na ni viashiria vya hatari. Kama hatua za haraka zisipochukuliwa mama na mtoto hupoteza maisha.
Jambo jingine linaloweza kusababisha hatari kwa mjamzito ni baadhi ya dawa muhimu za malaria kupigwa marufuku asizitumie.
Hii inatokana na baadhi ya dawa kuwa na madhara kwa mimba ambapo zikitumika kiholela huweza kusababisha kuharibika.
Hii ni kusema mama mjamzito hana wigo mpana wa kumtibu kwa dawa mbalimbali za malaria pale anapougua.
Je nini kifanyike?
Jambo la msingi ambalo mjamzito anapaswa kuzangatia ni kuhudhuria kliniki ambako ataelimishwa mambo mengi na atafanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara wa vihatarishi vya mimba ili vidhibitiwe mapema.
Kipindi cha ujauzito katika mahudhurio ya kliniki hupewa dawa za SP kama sehemu ya kumpatia mama kingatiba.
Hata hivyo kupatiwa kwa kingatiba hiyo hakumpi kinga ya asilimia 100 dhidi ya malaria bali kupunguza makali yake tu.
Kinga nyingine anayopatiwa ni chandarua maalum kilichowekwa dawa maalumu kumkinga asing'atwe na mbu wanaoeneza malaria.
Mama mjamzito pia hupatiwa dawa za madini ya chuma na minyoo ili kumuepusha na mambo ambayo yanaweza kumsababishai upungufu wa damu.
Mjamzito pia anapaswa kumuona mhudumu wa afya mapema pindi anapoona dalili kama kichwa kuuma, homa, kuumwa viungo vya mwili, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika, kuishiwa nguvu, kuona kiza ua kizunguzungu.
CHANZO:www.manyandahealthy.blogspot.com