Hiki ndio kilichonisababisha kupima VVU

Hiki ndio kilichonisababisha kupima VVU

Master SM

Member
Joined
May 29, 2020
Posts
55
Reaction score
54
Habari wana jamvi, natumai hamjambo. Niende moja kwa moja kwenye mada

Ilikua ni siku ya alhamisi shuleni x nilipokua A - level mida flani hivi ya jioni nimetoka zamgu kupiga kujisomea narudi bwenini, kuingia kwenye room ninapolala nikakuta kuna ugomvi wa masela wawili wote wa ile room.

Kwakua wote ni wadau tunaishi pamoja nikaona sio mbaya niwaamulie, HAPA ndipo kizaazaa kikaanza. Nilipoamua kuingilia ugomvi badala ya kusuluhisha nikashanga ugomvi umehamia kwangu, mmoja kati kati ya wale wana room akaanzisha vurugu kwangu kiasi kwamba ni kama alikua anagombana na mimi.

Vurugu ilikeisha juu kwa juu kila mtu akawa na mishe zake kama kawaida.

Kesho yake (ijumaa) asubuhi ndio balaa lilinipata, nilikua kwenye harakati za kujiandaa kwenda darasani ghafla nikachomwa na pini( zile za daftari) kwenye kidole, sikushtuka sana japo damu zilitoka kwahio nikapotezea. Nikasepa zangu darasani, ilipofika jioni nilianza kuona tofauti mwilini mwangu

Nilianza kuhisi miguu imekua ya baridi sio kawaida, kichwa kikawa kinauma, nilikua na wasiwasi kiasi ila siku ilipita.

Weekend yote sikua na mana niliendelea kuhisi baridi ambayo sio ya kawaida (miguuni) pekee, jumatatu tulikua tunaanza mitihani ya kanda, nikiwa kwenye chumba cha mtuhani nilijiona wa tofauti vidoleni niliona vidole vilisinyaa tofauti na nilivyokua mwanzo,

Nilifanya mitihani ile nikiwa na msongo mzito wa mawazo huku najiuliza nimepatwa na tatizo gani, ndani ya siku chache kulikua na walioniunishanga kwakua nilikonda ghafla, mm mwnyewe nilikua shahidi wa hayo, moyoni nikiwa na maswali mengi,

Siku ya mwisho ya mitihani ile nilijitafakari kisha nikaona niende hospitali kupima ngoma mana nilikua naona ntakata moto nikichukulia mzaha afya yangu.

Nilienda hospitali ikachukuliwa sample ya damu, nikiwa nasubiri majibu zilikuja fikra kichwani( HIVI NIKIKUTWA NAO NITAISHIJE ) nikataka kuyakimbia majibu ya vipimo, nilipokuja kukumbuka kilichonipeleka, niliona nitulie tu liwalo na liwe,

Ghafla nikasikia nimeitwa kupokea majibu, vipimo vilionyesha yalionyesha nilikua mzima tu.

Na hii ndio sababu yamimi kwenda hupima Vvu kwa hiari, kwa upande wako ni kipi kilikufanya ukaenda kupima?

Na kama bado unahisi lipi litakushawishi ukapime, share hapa na wanajamvi.

Wasalam
 
Ulipaniki tu bila sababu.Ngwengwe haimshambulii mtu kwa haraka hivyo.Haiwezekani uipate leo halafu wiki moja baadaye ioneshe dalili,nope.
 
Wenzio tushapima mpaka tumechoka, yani ukikumbuka Ile make amepata ujauzito halafu ukumbuke ilivyokuwa chuoni unzoa wale madada maarufu wa huduma pendwa na unapiga mbichi aisee ilikuwa shida. Hii tunaongelea miaka 14 iliyopita.

Kwa sasa najilia mbichi tu umri umeshaenda na dawa zipo hata kifo kikija Cha ukimwi no miaka 20 ijayo ambapo itakuwa ni sawa na natural death tu. Maana hata nisipoumwa ngoma nitakuwa na magonjwa ya uzeeni kibao.
 
Nilitakiwa kwenda mchangia mtu damu. Nikajiwahi kimya kimya.
 
Mimi nikipata kazi mpya. Mnoko mmoja akasema lazima niende Hindu mandal kupima.
Kupima sio issue. Mitihani iko kwenye kusubiri matokeo.
 
Kwamba ulipima ukimwi ulioambukizwa ndani ya wiki[emoji849][emoji849][emoji849],ulikuwa unawaza nini!!
 
Back
Top Bottom