Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 738
- 273
Ukiwa unatokea Masaki, kwenye makutano ya barabara za Haile Selassie na Ali Hassan Mwinyi, jirani na Kanisa la Mt. Petro, Oysterbay, Dar es Salaam, pana taa za kuongozea magari. Kwa pembeni, pana kibanda ambacho hutumiwa na askari wa usalama barabarani kujikinga na jua. Sasa, kwa muda mrefu, pamekuwa na askari, ama wenye sare za "trafiki ", au wenye silaha za moto, ambao kazi yao kuu ni kuangalia magari yanayotoka upande wa Masaki, na kuhakikisha wanabaini kuwa dereva ana makosa. Baada ya hapo dereva huelekezwa kupaki gari pembeni, kwenye hicho kibanda na baada ya mazungumzo mafupi au marefu, dereva huruhusiwa kuendelea na safari yake.
Sina hakika kama utaratibu huu hufanywa kwa halali. Kwa kifupi sehemu hiyo imekuwa kama kituo bubu cha polisi. Na shaka yangu yangu kubwa ni kuwa badala ya askari wenye silaha za moto kuwa makini na kufuatilia hali ya usalama katika mazingira yale, kwa ujumla wake, wao inavyoelekea, wamejikita katika kukagua magari na madereva wanaotoka upande wa Masaki.
Naomba hili nalo wakalitazame.