Hilda Newton: Hili liwe funzo kwa Mafwele na genge lake. Christopher Bagenyi kunyongwa hadi kufa

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
HILI LIWE FUNZO KWA MAFWELE NA GENGE LAKE.

SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo, it's over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!”​

​
 
Napendekeza abadilishiwe mkanda, apewe ule wa utambi, ikibidi iwe rahisi kwake kujichukullia sheria mikononi kwa manufaa mapana zaidi ya yatıma na wajane aliozalisha kwa tamaa za vipande vya dhahabu... kenge kweli
 
Mbona mazingira ya madai ya Hilder na maamuzi ya hiyo kesi haviendani.

Chadema huwa wana kawaida ya kuweka vilio vyao kwenye kila jambo hata kama havina uhusiano.
 
Hii habari imenikumbusha wale waliotaka kumteka yule Bonge kule mbezi/Kimara

Wale nao walitumwa na maboss zao ambao ni polisi

Walikuwa na ka "genge" kao ka kiharamia ambako ndani yao wamo polisi kadhaa, na wahuni wengine kama mabondia na matapeli wa mjini

Hao tuachane nao, tuzungumzie polisi wanaokubali kuunda hayo magenge na kutumika na wakubwa

Katika lile kundi lililokamatwa baada ya kushindwa kumteka "Bonge" yule, walikuwemo polisi kadhaa lakini kwasababu walikamatwa na polisi wenzao na waliotakiwa kutoa taarifa ni polisi wenzao, walificha huo utambulisho wao

Mmoja wapo namfahamu toka utotoni na ni miongoni mwa waliohukumiwa miaka saba jela

Nikiwa na ndugu zake huwa nawaonea huruma sana wanavyohangaika toka anakamatwa mpaka alipohukumiwa

Kwanza ni dogo aliyetoka familia masikini, lakini kwake alikuwa ameshajitengenezea utajiri (kwa maisha yake na alipotoka, aliokuwa nao ni utajiri kwasababu hakuna hata mmoja kwenye familia yake anayemiliki mali anamiliki)

Lakini kwasababu ya tamaa zake, sasa hivi yupo gerezani, hakuna mkuu wake anayehangaika nae, hakuna rafiki anayehangaika nae. Yuko peke yake

Mwanzoni akiwa bado hajahukumiwa naskia alikuwa anajigamba kuwa hawezi kufungwa akitarajia wakubwa zake watampambania atoke

Ilifikia hatua akiwa bado mahabusu alikosana na baadhi ya marafiki na ndugu zake walioonyesha masikitiko yao kwa kujua vitendo alivyokuwa najishughulisha navyo kwasababu tu alikuwa anamiliki siraha na gwanda za polisi

Akimaliza kifungo chake atarudi uraiani akiwa hana kazi maana yake ataanza upya

Pengine akishakuwa raia wa kawaida, aliowadhurumu na kuwatendea vibaya wataendelea kumtafuta ili kulipiza kisasi

Hapa duniani sote tuna pita, tutendeane wema hakuna haja ya kuumizana wakati hatujui kesho yetu
 
Duuuh 🥺🥺🥺🥺
 
Picha ya lini hii? Mbona amenawiri kama mtu ambaye hayuko jela?
 
Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu.
Na hao je wanaowatuma walio chini yao?

Kwa nini na wao yasiwahusu hata zaidi ya haya aliyopewa huyu. Bagenda!
 
Hanyongwi mtu hapo, Bongo ni ile ile ya Oct'29. Toothless Forces
 
Mbona mazingira ya madai ya Hilder na maamuzi ya hiyo kesi haviendani.

Chadema huwa wana kawaida ya kuweka vilio vyao kwenye kila jambo hata kama havina uhusiano.
Si Bora kwa sasa wana huo udhaifu wa kuweka vilio!
Nyakati zinakuja vilio vitakoma.
Utaratibu utakuwa ni jino kwa jino!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…