BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mimi ni mkazi wa Jirani na shule hiyo, kuna Dampo kubwa lililojaa uchafu na kutokana na upepo na Wanyama wengine kupita eneo hilo, kumekuwa na uchafu mwingi unaosambaa na kuwa kero zaidi kwa wapita njia.
Shule hiyo Kongwe iliyopo katikati ya Mji wa Babati, pamoja na uwepo wa Dampo ilo lilijaaa uchafu mwingi haina uzio, hivyo hakuna utulivu kwa Wanafunzi na wala uchafu wenyewe unaozagaa hapo.
Upande mmoja shule hiyo imepakana na uwanja wa mpira wa miguu na Stendi ya Zamani ambapo kwa sasa ni inatumika kama Soko.