mandarijunior
Member
- Feb 14, 2017
- 33
- 37
KATIKA Misimu minne ya ligi kuu Tanzania bara kuanzia 2012, Young African SC tumetwaa taji mara 3 na Azam FC 1, Msimu huu panapo majaaliwa itakuwa mara yetu ya tatu mfululizo . . Inasikitisha kuona ndugu zetu wamekuwa wakipambana kutafuta ushindi kupitia kamati! Waliwahi mchezesha Ibrahim Ajib akiwa na kadi 3 za njano, Walimchezesha Novalty Lufunga ambaye alikuwa ana kadi nyekundu lakini yote haya kwao yalipita kama upepo, wakabadili sheria na utaratibu wa ligi ili kujikinga makosa yao. . Kwa Ajib wakasema ni ruksa mchezaji kuchagua michezo na kwa Lufunga wakadai rufaa imecheleweshwa maisha yakaendelea.
Leo mchana kamati ya masaa 72 ilikaa, ilijadili rufaa ya klabu ya Simba wanaolalamika kuhitaji wapewe alama 3 kwa kuwa Kagera Sugar walimchezesha mchezaji mwenye kadi 3 za njano, mvutano ulikuwa mkubwa na kufanya kamati hiyo kushindwa kutoa maamuzi leo hadi siku ya alhamisi. . Jambo lililowazi ni kuwa mchezaji huyo kadi moja ni ya kombe la shirikisho sio ligi kuu lakini cha kusikitisha watani zetu wanajaribu kupindua pindua sheria ili tu wapate hizo alama 3, Ndio maana wameamua kujipa muda waweze kujitengenezea sheria yao.
Kwa hili Wana- Yanga hatutokubali kamwe, tumetumia gharama kubwa kusajili wachezaji pamoja na walimu bora, timu imekuwa inaendeshwa kwa mazingira bora yote hiyo ni kuhakikisha tunafanya vema katika michuano inayotukabili lakini wengiñe wanajifungia vyumbani kuandaa sheria kandamizi kwa kuwa tu wao wamekuwa na idadi kubwa ya wajumbe katika kamati.
Ni kamati hii hii hadi leo wameiweka kapuni rufani ya Yanga SC waliyowakatia African Lyon, kwa kumchezesha mchezaji Venance Ludovic, huku akiwa hajakamilisha taratibu zake za uhamisho kutoka Mbao FC ya Mwanza. Hizi ni pointi mbili za wazi ambazo Yanga wanastahili kupewa lakini swala limekuwa gumu tu kwa kuwa ni Yanga.
Watani zetu tunajua mna kiu ya Ubingwa lakini ubingwa haupatikani kwa njia hizo, mnatuvurugia na kuharibu ligi yetu na soka letu kwa ujumla kisa tu mtimize azma yenu ilhali mkijua uwezo wenu mdogo! Tucheze mpira taratibu na sheria husika ziamue lakini sio kwa ubabaishaji mnaoufanya.
SIKU NJEMA Mwananchi.
- Hissan Salum Iddi.