Habari wadau wa Elimu! Tangu siku ya leo ianze moja ya habari zilizoenea mtaani ni kuhusu ufutwaji wa matokeo ya kidato cha nne 2012 ambayo tume iliyoundwa na Waziri mkuu kubaini sababu za kufeli na kutoa mapendekezo ya nn kifanyike imeshakamilisha kazi yake, baada ya taarifa yao serikali imeamuru baraza kufuta matokeo na kusahihisha mitihani upya kwa kujitetea na kutoa sababu lukuki likiwemo la upangaji wa madaraja, yapo mambo kadhaa ninayojiuliza kama kweli yaweza kuwa suluhu ya janga hili katika Elimu;
1:Hivi baraza la mitihani ni akina nani? hiki si kitengo tu katika Wizara ndani ya serikali hiyohiyo! kama ndiyo walikuwa wapi kustuka kwa hili kabla ya matokeo? au kwa kuwa waliofelishwa ni wengi kuliko miaka mingine, na vipi kwa waliofelishwa miaka mingine kwa taratibu zenu binafsi maana kuna wahanga wa hili wengi sana na bado wapo mtaani na wengine wanaendelea kutafuta Credit kwa kufanyiwa maksudi haya. au mpo kibiashara kwa malipo ya ada za mitihani?
2:Kufuta matokeo na kusahihisha upya ndo litaondoa tatizo la Elimu nchini? au mnakwepa hoja za wapinzani
Tatizo si kusahihisha upya wala madaraja, ni Mfumo mbovu wa mitaala ya Elimu,uduni wa maslahi kwa Walimu, miundombinu mibovu ya Elimu Tanzania,ukosefu wa walimu na kushuka kwa maadili.